AFIKISHWA MAHAKAMANI MPANDA KWA TUHUMA ZA KUDHURU MWILI
Na.Boniface
Mpagape-Mpanda
MTU
mmoja mmoja mkazi wa Kasokola wilayani Mpanda Bw. Godfrey Kipyela, jana
amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo mjini Mpanda akikabiliwa na shtaka la
kudhuru mwili.
Akisoma
shtaka hilo, KIoplo Mtei wa jeshi la polisi Mpanda amesema mshtakiwa alitenda
kosa hilo tarehe 13 desemba mwaka 2015, saa moja usiku maeneo ya Kasokola
ambapo alimshambulia Bi. Maria January kwa kumpiga ngumi maeneo mbali mbali ya
mwili na kumsababishia maumivu makali.
Hakimu
wa mahakama ya Mwanzo mjini Mpanda Bw. David Mbembela baada ya kusikiliza
maelezo ya mlalamikaji pamoja na ushahidi uliotolewa na mtoto mdogo mwenye
umria wa miaka sita, amesema mlalamikaji anapaswa kuwasilisha mahakamani hati
ya matibabu yenye muhuri kutoka hospitali alikopatiwa matibabu.
Kesi
hiyo itasikilizwa tarehe 21 mwezi huu, na dhamana dhidi ya mshtakiwa inaendelea.
Comments