WATATU KATA YA MPANDA NDOGO WAFIKISHWA MAHAKAMANI MPANDA WAKITUHUMIWA KUJIPATIA SHILINGI MIL.3,400,000/= KWA NJIA YA UDANGANYIFU
Na.Issack
Gerald-Mpanda
WATU
wawili wakazi wa kata ya Mpanda ndogo wilayani Mpanda mkoani Katavi, jana
wamefikishwa katika mahakama ya mwanzo mjini Mpanda wakikabiliwa na shtaka la
kujipatia fedha shilingi milioni tatu na laki nne kwa njia ya udanganyifu.
Mlalamikaji
Bw. Lyango Joseph Mkazi wa Katumba ameiambia mahakama hiyo kuwa washtakiwa
Mustafa Mfaume na Mohamed Salum walitenda kosa hilo la kujipatia fedha kwa njia
ya udanganyifu kati ya mwaka 2014 na 2015.
Mbele
ya hakimu wa mahakama hiyo Bw. David Mbembela, mlalamikaji Bw. Lyango Joseph
amesema kuwa, mshtakiwa namba moja ambaye ni Bw. Mustaph Mfaume mnamo tarehe 20
mwezi desemba mwaka 2014 alienda nyumbani kwa Lyango Joseph na kuomba shilingi
laki nne kwa lengo la lengo la kufanyia shughuli za kilimo cha tumbaku katika
maeneo ya Kapemba kwa ahadi kuwa akiuza tumbaku atarudisha fedha alizokopa bila
riba.
Mlalamikaji
Bw. Lyango Joseph ameiambia mahakama hiyo kuwa mnamo tarehe 16 mwezi januari
mwaka 2015 mshtakiwa namba moja aliongeza tena ombi la kukopeshwa shilingi laki
nne kwa lengo lile lile. Amesema mnamo tarehe 05 mwezi februari mwaka 2015
aliomba akopeshwe tena shilingi laki tatu kwa ahadi ya kurejesha atakapouza
tumbaku.
Mlalamikaji
ameendelea kuiiambia mahakama ya mwanzo mjini Mpanda kuwa, mnamo tarehe 23
mwezi April mwaka 2015 mshtakiwa Mustafa Mfaume, aliomba tna akopeshwe shilingi
laki sita lwa lengo lile lile la kuendeleza kilimo cha zao la tumbaku.
Bw.
Lyango amesema mwezi April mwishoni tarehe ambayo mlalamikaji haikumbuki,
mshtakiwa namba moja Bw. Mustafa Mfaume alikwenda tena nyumbani kwa mlalamikaji
Kanoge ambaye ni rafiki yake wa muda mrefu na kuomba tena shilingi laki mbili
ili aendeshee kilimo cha tumbaku na alikopeshwa fedha hizo na mwishoni mwa mwezi
Mei tarehe ambayo mlalamikaji haikumbuki mshtakiwa namba moja Bw. Mustafa
Mfaume alimpeleka mshtakiwa namba mbili Bw. Mohamed Salum na kuomba amdhamini apewe shilingi laki mbili
lakini mlalamikaji Bw. Lyango Joseph alikataa kwa kuwa hamfahamu na ndipo
Mshtakiwa Mustafa Mfaume akadai anamdhamini, na kutokana na ukaribu na urafiki
wao alikubali na kumkopesha kiasi hicho cha fedha.
Mlalamikaji
amesema kwa mara ya mwisho mshtakiwa Mustafa Mfaume alikwenda kwake tarehe 12
mwezi Mei na aliomba fedha shilingi milioni moja na laki mbili ili zitumike
kwenye shamba lake la tumbaku na kuahidi atakapouza na kupata malipo atarejesha
fedha hizo bila riba.
Mlalamikaji
Bw. Lyango Joseph amesema mshtakiwa namba moja Bw. Mustafa mfaume alikuwa
amejipatia jumla ya shilingi milioni tatu na laki mbili na mshtakiwa namba mbili
Bw. Mohamed Salum alijipatia shilingi laki mbili na kufanya jumla kuu ya fedha
walizojipatia kwa udanganyifu kuwa shilingi milioni tatu na laki nne.
Awali
washtakiwa wote wawili walitiwa hatiani na mahakama hiyo na kuhukumiwa kifungo
cha miezi sita jela kutokana na kukiri kosa la kujipatia pesa kwa njia ya
udanganyifu toka kwa Bw. Lyango Joseph na hukumu hiyo iliwataka watakapomaliza
kutumikia adhabu ya kifungo jela, warejeshe fedha kwa mlalamikaji lakini baada
ya kutoka jela hawakutekeleza amri ya mahakama
ya kumlipa mlalamikaji.
Mlalamikaji
katika shauri hilo Bw. Lyango Joseph ametoa pia vielelezo vya hati 6 walizoandikiana
pamoja na nakala ya uamuzi wa mahakama uliowatia hatiani washtakiwa. Washtakiwa
wamekubali vielelezo vyote vilivyotolewa mbele ya mahakama ya mwanzo mjini
Mpanda.
Hakimu
wa mahakama hiyo Bw. David Mbembela amesema kwa kuwa washtakiwa hawajapinga
nakala ya uamuzi wa mahakama iliyowatia hatiani, hata hivyo hati 6 zilizotolewa
mahakamani kama kielelezo mahakama imezikataa mpaka zithibitishwe na kamishna
wa viapo ili ziweze kutambulika kisheria kuwa ni hati halali.
Kesi
hiyo imeahirishwa hadi tarehe 03 mwezi Februari mwaka huu, kungoja ushahidi
kutoka kwa washauri wa mahakama waliosikiliza kesi hiyo tangu mwanzo ambapo
hata hivyo hamimu Mbembela amesema dhamana kwa washtakiwa zinaendelea.
Comments