WAZIRI MKUU AELEZA MIKAKATI YA SERIKALI KUFUNGUA VIWANDA VYA NGOZI DAR, GEITA NA SHINYANGA
Issack Gerald-DAR ES SALAAM
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema,Serikali imepanga kufungua viwanda vya kusindika
ngozi kwenye mikoa ya Shinyanga, Geita na Dar es Salaam ili kutoa soko kwa
ngozi za wanyama wanaochinjwa kwenye machinjio ya mikoa hiyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watanzania waishio Botswana baada ya kuhudhuria mkutano wa SADC mjini Gaborone Januari 18, 2016. Waziri |
Majaliwa
ametoa kauli hiyo jana jioni wakati akizungumza na baadhi ya Watanzania waishio
Botswana kwenye kikao kilichofanyika kwenye kituo cha mikutano ya kimataifa
(GICC), jijini Gaborone, Botswana.
Waziri
Mkuu amekuwa nchini Botswana kwa ziara ya siku moja kumwakilisha Rais Dk. John
Pombe Magufuli kwenye mkutano wa SADC Double Troika yaani kikao maalum cha
Wakuu wa Nchi na Serikali na Wakuu wa Nchi wanaounda Chombo cha Ushirikiano wa
Siasa,Ulinzi na Usalama.
Amesema
Serikali imeamua kuongeza viwanda nchini, kama njia mojawapo ya kukuza uchumi,kuacha
kuuza mali ghafi lakini pia ni fursa ya kuongeza ajira kwa Watanzania.
Wakati
huo huo akijibu hoja zilizoainishwa kwenye risala yao, Waziri Mkuu Majaliwa amesema
Serikali bado ina nia ya kuhamia Dodoma na kwamba itaendelea kutenga fedha
zaidi ili wizara nyingi zijenge ofisi zao Dodoma.
Aidha
Waziri Mkuu Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwataka Watanzania waishio ughaibuni kutafuta
fedha za mitaji ambapo fedha hizo zinaweza kuwa zao au kupitia kwa marafiki zao
ili waweze kuwekeza nyumbani Tanzania.
Awali
akisoma risala yao kwa niaba ya wenzake, Mwenyekiti wa Chama cha Watanzania
waishio nchini Botswana Bw. Neiman Kissasi amesema chama hicho kilianzishwa
mwaka 1992 kikiwa na lengo la kuwaunganisha Watanzania waishio Botswana pamoja
kujenga undugu wao na kusaidiana.
Katika
risala yao, wameshauri wafugaji wa Tanzania waelimishwe na kuwezeshwa kufuga
kisasa na kuondokana na ufugaji wa kurandaranda.
Vilevile,
wameiomba Serikali ifungue fursa za kiuchumi kwenye mikoa mingine ya Tanga,
Lindi, Mtwara, Pwani, Kigoma, Mbeya, Mwanza na Arusha badala ya kuziacha ziwe
Dar es Salaam peke yake.
Waziri
Mkuu amerejea jijini Dar es Salaam jana usiku.
Chanzo cha habari : Ofisi ya Waziri Mkuu
Comments