KATAVI YAPOKEA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 80 ZA KUGHARIMIA ELIMU BURE.
Na.Issack Gerald-Katavi
Mkoa wa Katavi umepokea Zaidi ya
Shilingi Milioni 80 kwa ajili ya kugharimia mpango wa serikali wa elimu bure
kwa wanafunzi kuanzia Chekechea hadi
kidato cha nne.
Kaimu Afisa elimu Sekondari Mwalimu Said Mwapongo amesema kuwa Mkoa wa
Katavi umepokea zaidi ya milioni 80 na tayari zimesambazwa katika shule kwa
ajili ya matumizi yaliyokusudiwa.
Afisa elimu Mwapongo,pamoja na kutoa
wito kwa jamii,anatolea ufafanuzi wa michango hiyo ambayo imefutwa pamoja na
ile inayopaswa kuchangwa.
Kuhusu wanafunzi waishio shule za
bweni ambazo ni za Kata,Mwapongo amesema kuwa ziko kwenye mpango wa serikali wa
kuziondolea michango inayotoka kwa wazazi kutokana na mpango wa wanafunzi
waishio bweni kuwa katika mipango ya wazazi,walimu na bodi za shule.
Ufafanuzi huo wa Kaimu Afisa Elimu
umekuja kufuatia malalamiko ya baadhi ya wazazi wakihoji kulikoni wanafunzi
waendelee kuchangishwa michango ya vitu mbalimbali kama vyakula,pesa ya mlinzi
na mpishi.
Mmoja wa wakazi kutoka kijiji cha
Kabulonge Kata ya Litapunga Wilayani Nsimbo ambaye hakutaka jina lake
litajweanasema yeye amekuwa na maswali mengi baada ya mtoto wake aliyeko katika
Shule ya sekondari machimboni kuanmbiwa atoe michango wakati mtoto wake
akipelekwa kuanza kidato cha kwanza.
Hata hivyo baadhi ya wazazi,walezi na
jamii kwa ujumla imeonekana kutoelewa vizuri mchanganuo wa michango iliyofutwa
na ilea ambayo jamii inapaswa kuendelea kuchagia.
Kwa Upande wake Afsisa elimu
Sekondari Manispaa ya Mpanda Bi.Enelia Lutungulu amesema kuwa kesho wanatarajia
kukutana na bodi za elimu kwa shule zilizo katika kata za Magamba,Kasokola na
Shanwe kwa ajili kuweka sawa mazingira ya utekelezaji wa sera ya elimu bure.
Katika fedha hiyo Wilaya ya Mlele
imepata zaidi ya Shilingi Milioni 32 kwa ajili ya elimu za msingi na sekondari na huku hesabu ya kujua kiasi
kilichopokewa kwa upande wa Wilaya ya Mpanda na Nsimbo kikiendelea
kuchanganuliwa vizuri.
Idara ya elimu sekondari Mkoa wa
Katavi kwa Ujumla imesema kuwa,wanaendelea kuweka mikakati ili kuhakikisha
wanashika nafasi ya juu katika mithani ya taifa kwa ngazi ya shule za sekondari
kama ilivyo kwa shule za Msingi ambapo Mkoa wa Katavi umeshika nafasi ya kwanza
kwa mwaka 2015 huku Manispaa ya Mpanda ikishika nafasi ya kwanza kitaifa kwa
miaka 2 mfululizo yaani mwaka 2014 na 2015.
Kwa mjibu wa barua ya tarehe 23
Novemba mwaka 2015 iliyoandikwa na Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi na
kusambazwa katika shule zote hususani za Sekondari Tanzania bara,inamtaka kila
Mkuu wa shule kumpatia mwanafunzi fomu iliyotolewa na Wizara na siyo ile
iliyokuwa ikiandaliwa na bodi au kamati za shule na lengo kuu likiwa kuondoa
migogoro ya michango ya shule moja kutofautiana na shule nyingine Wakati huo
huo barua ya Novemba 27 mwaka 2015 ikiainisha wajibu wa
mzazi,mlezi,mwalimu,bodi au kamati za shule na jamii kwa ujumla.
Comments