RADI YAUA WAWILI YAJERUHI WATATU KATAVI
Na.Issack
Gerald-Katavi
Watu wawili waliofahamika kwa majina ya Kupiwa
Julius (28) na Lemmy Madirisha wote wakazi wa Mkazi wa Ilebura wamepigwa na
radi na kufariki dunia papo hapo.
Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhairi Kidavashari
amesema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa nane na nusu mchana katika
kijiji cha Ilebura Tarafa ya Kabungu Wilaya ya Mpanda.
Amesema kuwa,katika tukio hilo,watu watatu waliojeruhiwa
wametajwa kuwa ni Tatu Gerald (28),Stela John (38) na Philbert Paschal wote wakazi
wa kijiji cha Ilebura.
Aidha kamanda Kidavashari amesema,kabla ya
tukio marehemu na majeruhi kwa pamoja walikuwa shambani wakilima ambapo wakati wakiendelea
kulima mvua ilianza kunyesha ambapo wote waliamua kwenda chini ya mti kujikinga
na mvua na ndipo radi ilipopiga na kupelekea madhara hayo.
Ameongeza kuwa baada ya tukio hilo majeruhi
wote wamepelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda na wanaendelea na
matibabu huku miili ya marehemu ikiwa imekabidhiwa kwa ndugu zao kwa ajili ya
mazishi.
Hata hivyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi anawatahadharisha
wananchi wote kuwa makini katika kipindi hiki cha masika pindi mvua
zinaponyesha kwa kujihifadhi maeneo salama ilikuepukana na madhara kama haya
ambayo huadhiri ustawi wa afya na uhai wa watu.
P5 TANZANIA MEDIA inatoa pole kwa ndugu jamaa
na marafiki waliofikwa na msiba na mungu awaponye majeruhi warudi katika hali yao
ya afya kama kawaida.
Comments