WAKAZI KATAVI WATAKIWA KUWA MAKINI NA MVUA KUEPUKA MAFURIKO PIA IDARA ZA MAAFA KATIKA HALMSHAURI ZOTE ZAAGIZWA KUJIPANGA KIKAMILIFU
Na.Boniface Mpagape-Mpanda
MKUU
wa Mkoa wa katavi Dk. Ibrahim Msengi amewataka wakazi wa mkoa huo,kuchukua
tahadhari kutokana na uwezekano wa kuwepo kwa mafuriko kama ilivyotabiriwa na
wataalam wa hali ya hewa.
Mkuu
wa mkoa wa Katavi ametoa tahadhari hiyo wakati akizungumza na Mpanda radio
ofisini kwake sambamba na P5 TANZANIA
MEDIA.
Amesema
wakazi wa mkoa wa Katavi wamekuwa wakijenga katika maeneo ambayo hayaruhusiwi
kwa makazi na kuwataka wawe katika maeneo yasiyo hatarishi.
Amewaagiza
wakurugenzi, na wakuu wa wilaya zote mkoani Katavi kwa kushirikiana na kamati zao za maafa
kujiandaa kikamilifu kwa kutoa tahadhari kwa wananchi ili kukabiliana na maafa
yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua za El-Nino.
Comments