AMPA UJAUZITO DADA YAKE WA MIAKA 14 SUMBAWANGA POLISI WAMDAKA,IDARA YA ELIMU NAKO KALAMBO HARAKATI KWA KWENDA MBELE
Na.Issack Gerald-Sumbawanga
POLISI wilayani
Sumbawanga Mkoani Rukwa inamshikilia mkazi wa kijiji cha Ulinji, Manispaa ya
Sumbawanga mwenye umri wa miaka 28 kwa tuhuma za kumpa ujauzito dada yake
mwenye umri wa miaka 14 anayesoma darasa la saba.
Inadaiwa kuwa
mtuhumiwa ambaye amemtaliki mkewe, alirejea kuishi nyumbani kwa wazazi wake
kijijini Ulinji miaka miwili iliyopita kabla ya kumpatia ujauzito mtoto huyo wa
baba yake mkubwa.
Polisi
imethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kwamba alikamatwa na Ofisa
Mtendaji wa Kijiji cha Ulinji, Manispaa ya Sumbawanga, Linus Mbutu.
Ofisa Mtendaji
wa Kijiji cha Ulinji, amesema mtuhumiwa amekamatwa juzi na askari wa Mgambo wa
kijiji hicho akiwa amejificha kwa saa tatu porini akikwepa kukamatwa.
Katika hatua nyingine,idara
ya elimu wilayani Kalambo mkoani Rukwa jana
imefanya kikao cha kujadili upungufu wa madawati uliopo wilayani humo.
Akizungumza na P5
TANZANIA MEDIA sambamba na mpanda radio kwa njia ya simu afisa elimu vifaa
na takwimu wa halmashauri ya wilaya ya Kalambo
Bi. Toba Mwihanga ameziomba taasisi
mbalimbali kutoa msaada ili kutatua changamoto hiyo.
Bi. Mwihanga amesema mwaka
2014 walipokea madawati 100 ambayo hayakukidhi mahitaji ya wanafunzi.
Aidha ameitaka jamii
kuendelea kushiriki katika ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu na vyoo,huku
akiwataka watendaji wa kata kuhamasisha jamii juu ya elimu bure , na kuiomba
serikali kuongeza walimu katika mkoa huo.
Comments