WANAOGOMBANIA ARDHI NSIMBO WATAKIWA KUTOKA,ELIMU BURE BADO KUELEWEKA IPASAVYO KWA WANANCHI MKUU WA WILAYA YA MLELE ATOA NENO
Na.Agness Mnubi-Nsimbo.
WADAU
wa Elimu katika halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi wametakiwa
kuelimisha wazazi na walezi juu ya Mfumo wa elimu bure.
Wito
huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Mstaafu Issa Suleiman Njiku
katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika jana katika Halmashauri ya
Wilaya ya Nsimbo, mara baada ya madiwani wa halmashauri hiyo kuhoji juu ya
Mfumo wa elimu bure.
Amefafanua
kuwa ni wajibu wa Mkurugenzi kuitisha kikao cha wadau wa elimu ili kuwaelimisha
wazazi na walezi juu ya Mfumo wa elimu
bure.
Aidha
amesema taarifa juu ya elimu bure
zibandikwe kwenye mbao za matangazo, ili kurahisisha kusambaza elimu hiyo na
kuwataka madiwani wa halmashauri ya Nsimbo kutoa taarifa za walimu wanaotoza
ada na mahitaji mengine ya wanafunzi ambayo yanagharimiwa na serikali.
Wakati huo huo,idara
ya Maliasili na Misitu katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo imeagizwa kutatua
mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa kata ya Urwila na kata ya Katumba, kuhusu
kilimo katika eneo la Nzaga ambalo ni
chanzo cha mto.
Kanali
Njiku ameongeza kuwa,wananchi wa Vijiji hivyo wanagombania kulima katika mpaka
wa eneo la mto, kinyume cha sheria na kufafanua kuwa sheria inaelekeza shughuli
za kibinadamu kuanza umbali wa mita 60 kutoka chanzo cha maji.
Kufuati
hali hiyo, amewataka wananchi wanaoishi katika misitu na hifadhi ya serikali, kuhama
na kuacha tabia ya kukata misitu na kuendesha shughuli yoyote katika hifadhi za
serikali.
Comments