ACHOMWA KISU WILAYANI MPANDA UTUMBO WATOKA NJE,MHUSIKA ATOKOMEA KUSIKOJULIKANA POLISI KUMSAKA MHUSIKA.
Na.Issack
Gerald-Katavi
Mtu
mmoja aliyejulikana kwa jina la Elia Edward(40), makazi wa mchangani alichomwa
tumboni na kitu chenye ncha kali na kisha utumbo wake kutoka nje na mtu asiyemfahamu.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo,Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari
amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo tarehe 24.01.2016 majira ya saa 19:00
jioni katika eneo la Mzabwela Kijiji cha Mchangani Kata ya Ikola Tarafa ya Karema
Wilayani Mpanda Mkoani Katavi.
Taarifa
ya Kamanda kidavashari inataarifu kuwa mara baada ya mtuhumiwa kutenda kosa la
kumchoma kisu majeruhi alikimbilia kusikojulikana.
Amesema
,majeruhi amepelekwa katika hospitali ya Wilaya Mpanda kwa matibabu zaidi huku Chanzo
cha tukio hili kikiwa bado hakijajulikana
Hata
hivyo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji cha mchangani
linamsaka mtuhumiwa alipokimbilia.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Katavi anatoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia
sheria mikononi ambapo amesema kuwa sheria kali zitaendelea kuchukuliwa pale
wahusika watakapobainika.
Comments