BREAKING NEWS : WAHAMIAJI HARAMU 8 RAIA WA ETHIOPIA WANASWA IRINGA-P5 TANZANIA INAKUSOGEZEA HIYO
Na.Issack Gerald-Iringa
Jeshi la polisi Mkoani Iringa
limewakamata wahamiaji haramu 8 Raia wa Ethiopia waliokiuwa wakisafiri isivyo
halali na bila kibali cha kuingia nchini wakiwa wamepakiwa na gari lililokuwa
limebeba magazeti.
Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa Peter Kakamba |
Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa Peter
Kakamba amesema kuwa watu hao wamekamatwa katika kituo cha ukaguzi wa magari
mvilo Manispaa ya Iringa wakati Polisi likiwa kwenye oparesheni ya kawaida.
Kamanda Kakamba amewataja baadhi ya
wanaoshikiliwa na polisi kuwa ni pamoja na Godfrey Tanka (32) ambaye ni dereva
akisaidizana pia na Michael Japhet (37) wote wakazi wa Dar es Salaam.
Wakati huo huo mtu anayedhaniwa kuwa
msindikizaji wa gari hilo naye anashikiliwa na Polisi Mkoani Humo ili kubaini
kama alikuwa akisindikiza magazeti au watu hao.
Kwa upande wake mmoja wa
wasindikizaji amesema kuwa wamepakia watu hao baada ya kusimamishwa na wapiga
debe ambapo kwa maelezo ya watu hao wa Ethiopia walisema kuwa wanaelekea Mkoani
Mbeya.
Comments