MANISPAA YA MPANDA WANG’ANGA’NIA HOSPITALI YA WILAYA YA MPANDA IWE YAO,KAKESE YAONGOZA KWA MAAMBUKIZI YA UKIMWI
Na.Issack Gerald-Mpanda
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda
imesema kuwa mchakato wa kuhamisha Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kutoka katika
utawala wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda kuwekwa katika utawala wa Manispaa
unaendelea.
Hayo yamebainishwa na mganga mkuu wa
Manispaa Dk.Obed Mahenge kupitia kikao cha balaza la madiwani ambacho
kimefanyika jana katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda.
Kutokana na Manispaa kutokuwa na
Hospitali yake ya Manispaa,Wajumbe wa kikoa wameiomba manispaa ya Mpanda mchakato
wa kuhamisha hospitali katika utawal mmoja kwenda utawala mwingine ufanyike kwa
haraka ili kuwaondolea adha wananchi.
Kwa upande wake afisa anayehusika na
ukusanyaji wa damu salama Manispaa ya Mpanda Bi.Redgunda Mayorwa,amesem akuwa
kipindi cha mwezi Desemba mwaka jana
hadi Mwezi Januari mwaka huu,amesem akuwa kiasi ch adamu kilichokusanywa ni
UNIT 407.
Katika hatua nyingine ,Dk.Mahenge
amesema kuwa kata ya Kakese imeendelea kupata ongezeko la watu wenye maambukizi
ya Virusi vya Ukimwi ambapo kwa kipindi cha mwezi Desemba mwaka 2015 hadi
Januari mwaka huu,zaidi ya watu 40 wamegundulika kuathirika.
Hata hivyo wadau mbalimbali
wameshauri kuwa,kondomu,elimu ya kutosha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
viendelee kutolewa kwa wakazi wote wa Mkoa wa Katavi.
Mkoa wa Katavi una asilimia 5.9 ya
maambukizi ambapo imevuka kiwango cha asilimia kwa taifa,ambapo maambukizi
asilimia ya maambukizi ni salimia 5.1.
Hata hivyo kuna uwezekano wa aslimia
kuongezeka ikiwa utafiti wa vipimo vya uhakika utafanyika kwa kumekuwa na
ongezeko la watu wengi kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania Kuingia Mkoani
Katavi.
Comments