BALAZA LA MADIWANI MPANDA LAUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI,WAPOKEA TAARIFA NA KUJADILI CHANGAMOTO ZA WANANCHI.
Na.Issack Gerald-MPANDA
Balaza la madiwani Manispaa ya Mpanda
limetoa kauli ya pamoja kuunga mkono Juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dk.John Pombe Magufuli.
Kauli hiyo ya Madiwani,imetolewa jana katika mkutano wa balaza la pili la madiwani ambao umefanyika katika ukumbi wa
Manispaa ya Mpanda.
Kupitia hicho kilichokuwa kinalenga
kupokea na kujadili taarifa za kamati mablimbali,baadhi ya masuala yaliyobainishwa
ni pamoja na kujadili namna ya kutatua changamoto zinazoathiri wakazi wa
Manispaa ya Mpanda.
Baadhi ya changamoto hizi ni Upungufu na ukosefu wa
maji kwa baadhi ya maeneo ya Manispaa kama vile kata za Mpanda Hotel,baadhi ya
maeneo ya Ilembo.
Changamoto nyingine zilizopo ni,Huduma
duni za afya katika Hospitali na Zahanati,Mapambano dhidi ya maambukizi ya
virusi vya Ukimwi,miundombinu mibovu ya barabara zilizopo katika mipaka ya
Manispaa.
Awali Mstahiki meya wa Manispaa ya
Mpanda Mheshimiwa Willium Philipo Mbogo
akifungua kikao hicho cha pili cha balaza hilo kwa mwaka 2016 amesema kuwa miradi mbalimbali inatarajiwa
kutekelezwa kwa kipindi cha miezi sita iliyosalia ya mwaka wa fedha 2015/2016.
Pamoja na mambo mengine,amesema,
miradi hiyo ni pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani,kutatua
changamoto za elimu kwa shule za
Manispaa zikiwemo upungufu wa madawati pamoja na na kutekeleza mipango ya
serikali.
Hata hivyo wajumbe katika balaza
hilo,wameiomba manispaa kutatua changamoto za migogoro ya ardhi na kuainisha
thamani ya magari mawili ya Manispaa aina ya Scania yanayotarajiwa kuuzwa mwaka
huu 2016.
Wakati huo huo Suala la ukosefu wa
Maji kwa baadhi ya maeneo ya Manispaa ya Mpanda limeonekana kuwakasirisha
baadhi ya madiwani na hivyo kuhoji wajibu wa viongozi waliopewa kusimamia
usambazaji wa maji safi na salama ambao ni idara ya maji MUWASA.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Manispaa ya Mpanda ambaye kisheria katika balaza la madiwani ndiye katibu,ametoa
rai kwa madiwani kusambaza elimu kwa wananchi ili kuendeleza kupambana na
maambukizi ya Ukimwi ambayo huenda kama takwimu zikitolewa kuna uwezekano wa
kuzidi asilimia 5.9 ya maambukizi ya Ukimwi kwa sasa.
Katika hatu a nyingine Halmashauri ya
Manispaa ya Mpanda inatarajia kuuza magari mawili aina ya Scania huku magari mengine
yatakayouzwa hayajaainishwa ni magari mangapi na aina gani.
Kwa upande wa baadhi ya wananchi
Manispaa ya Mpanda wamesema kuwa miundombinu ya afya,barabara,afya maji na migogoro
ya ardhi inatakiwa kutatuliwa haraka.
Comments