WAZIRI WA KILIMO,MIFUGO NA UVUVI ZIARANI MLELE,ATOA RAI KWA WATUMISHI WA UMMA,AZUNGUMZA NA WAKULIMA WA TUMBAKU
Na.Issack Gerald-Mlele
Waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi
Mheshimiwa Willium Tate Nashe,amewataka watumishi wa umma Wilayani Mlele Mkoani
Katavi kufanya kazi kwa uadilifu,uaminifu sambamba na kuwa karibu na wananchi
kwa ajili ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi hao.
Waziri Nashe ametoa wito huo jana,
alipokuwa akizungumza na watumishi wa sekta mbalimbali Wilayani Mlele katika
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mlele.
Aidha,Nashe baada ya kikao na
watumishi wa Umma,aliendelea kuzungumza na Chama cha msingoi cha Ushirika cha
Ukonongo kinachojishughulisha na kilimo cha tumbaku.
Amebainisha malengo makuu ya ziara
yake aliyoianza Jumatatu ya Januari 11 mwaka huu,Mkoani Katavi kuwa ni kwa
ajili ya kuja kutatua changamoto za wakulima zinazowakabili katika sekta ya
kilimo,ardhi,ufugaji na uvuvi.
Wakati huo huo,ameupongeza mkoa wa
Katavi kwa kuwa miongoni mwa mikoa ambayo haina historia ya njaa kwa kuwa Mkoa
wa Katavi unalisha maeneo mengine yaliyokumbwa na njaa ikiwemo Shinyanga.
Waziri anaendelea na ziara ambapo leo
ni siku ya tano tangu aanze ziara Mkoani Katavi ambapo ameelekea Wilayani Mlele
akitokea Wilayani Mpanda baada ya kupata taarifa ya Mkoa ya maendeleo ya
kilimo,mifungo na uvuvi na hatimaye kuzungumza na wakulima wa tumbaku wa
chama cha msingi cha ushirika cha Mpanda kati.
Comments