MRAJISI VYAMA VYA MSINGI TANZANIA APEWA SIKU 14 KUUNDA TIMU YA UKAGUZI MALALAMIKO YA WAKULIMA WA TUMBAKU MPANDA
Na.Issack Gerald-Mpanda,Katavi
Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na
Uvuvi Mh.William Tate Ole Nasha,amemwagiza Mrajishi wa vyama vya
ushirika Tanzania,kuhakikisha anaunda timu ya ukaguzi ndani ya Siku 14 ili
kuchunguza malalamiko ya wakulima wa zao la tumbaku katika chama cha msingi cha
ushirika cha Mpanda Kati kilichopo Wilayani Mpanda.
Waziri Nasha ametoa agizo hilo katika
kikao ambacho kimefanyika katika ukumbi wa idara ya maji Wilayani Mpanda kikishirikisha
Viongoz I wa vyama vya ushirika Mpanda Kati,Kaimu mrajishi Mkoa,Mkuu wa Wilaya
ya Mpanda na viongozi wengine waandamizi amabo amekuja nao kutoka Wizarani.
Akizungumza mbele ya wanachama zaidi
ya 100 wa chama cha ushirika Cha Mpanda Kati,Waziri Nasha ameonesha
kutoridhishwa na majibu ya uongozi wa ushirika Wilaya ya Mpanda kutokana na
majibu yao kutokuonesha wazi taarifa za malipo ya pesa za wakulima.
Katika malalamiko ya wakulima ni
pamoja na kutolipwa pesa zao kwa awamu tofauti kutokana tumbaku yao
iliyouzwa,kupunjwa kwa pembejeo za kilimo,kulipwa kwa Shilingi badala ya Dola
kama wanavyoza na masuala mbalimbali kama amvyo baadhi wamebaoinisha.
Hata hivyo,kufuatia kauli ya serikali
kwa mrajisi wa vyama vya ushirika Tanzania kumtaka kuunda timu ya uchunguzi,wakulima
hao wamekuwa na maoni Tofauti kuzungumzia hatua hiyo.
Kwa nyakati tofauti wakulima wa chama
hicho cha msingi wamekuwa wakilalamika kunyanayaswa kutokana na uuzaji wa
tumbaku yao na malipo wanayopewa kuanzia miaka
ya 2010,ambapo kwa mjibu wa wakulima wametaka kufahamu Jumla ya shilingi
milioni 600 zilipo ili walipwe pesa zao.
Hata hivyo Afisa ushirika Wilayani
Mpanda Luxford Mbunda amesema kuwa hakuna pesa wanayodai wakulima wala wakulima
hao hakuna deni wanalodaiwa ambapo ndicho chanzo cha sokomoko la sintofahamu juu ya upatikanaji wa pesa hizo.
Viongozi wa Wilaya na Mkoa licha ya
kuwa wanatafuta ufumbuzi wa mgogoro huo hakuna mafanikio yaliyopatikana.
Chama cha Msingi cha Ushirika cha
Mpanda Kati,ni miongoni mwa vyama saba vya msingi vinavyounda chama kikuu cha Ushirika
LATCU Mkoani Katavi.
Awali Waziri alipokea taarifa ya Mkoa
katika sekta ya kilimo,mifugo na uvuvi kabla ya kwenda katika ukumbi wa idara
ya maji kaufanya kikao na wakulima wa tumbaku chama cha Mpanda kati.
Endelea kuhabarika na P5 TANZANIA MEDIA
Endelea kuhabarika na P5 TANZANIA MEDIA
Comments