CUBA YAENDELEA KUSAIDIA TANZANIA KUPAMBANA NA MALARIA
Na.Issack Gerald-Katavi
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini,
Bwana Jorge Luis Lopez Tormo ambaye ameahidi kuendelea kusaidia Tanzania katika
mapambano dhidi ya malaria.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo, ofisini kwake jijini Dar es slaam Januari 11, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) |
Akizungumza
na Balozi Tormo leo ,ofisini kwake ,Magogoni jijini Dar es salaa, Waziri
Mkuu amemshukuru Balozi huyo, kwa Serikali ya Cuba kuendelea kusaidia Tanzania
katika mapambano dhidi malaria kwa kusaidia ujenzi wa kiwanda
cha kwanza Afrika cha viuadudu vya kuua viluwiluwi wa mbu
wanaoeneza ugonjwa wa malaria kilichopo, Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani
kinachosimamamiwa na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC).
“Nawashukuru
sana kwa namna mnavyosaidia kupambana na malaria, kupitia mradi huo mkubwa
Afrika ambao unalenga kumaliza ugonjwa wa malaria,unaosababisha idadi kubwa ya
vifo katika nchi yetu.” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Pia,
ametumia fursa hiyo kuwakaribisha raia wa Cuba kuja kuwekeza nchini hasa
katika teknolojia. Na ameahidi kuendeleza uhusiano mwema
ulipo baina ya nchi hizi mbili.
Waziri
Mkuu ameendelea kwa kusema kuwa Cuba ni nchi iliyoendelea katika
biashara, viwanda na uwekezaji na imefanikiwa kutoa bure huduma za
kijamii ikiwemo afya, hivyo Serikali ya Tanzania haina budi kujifunza kutoka
kwao ili kutimiza azma yake ya kutoa bure huduma mbalimbali za kijamii kama
ambavyo sasa inatolewa elimu bure.
Kwa
upande wake, Balozi Tormo amesema kuwa pamoja na Serikali ya Cuba
kusaidia kutoa wataalamu katika kujenga kiwanda hicho cha viuadudu
vya kuua viluwiluwi wa mbu wanaoeneza ugonjwa wa malaria ambao utanufaisha pia
nchi za jirani siku za usoni, wanapenda kuendeleza ushirikiano na
Tanzania katika kuzalisha wataalamu kupitia programu mbalimbali ikiwemo
afya na elimu. Mfano progamu inayoendelea ya kubadilishana wataalamu
katika kitivo cha madawa cha Chuo Kikuu Cha Zanzibari (SUZA).
“Tunaweza
kuendeleza program za kujifunza lugha ya Kiswahili, kama hapo awali, hii ni
njia nzuri na muhimu ya kuendeleza uhusiano wetu na watu kuelewa lugha zetu”,
alisema Balozi Tormo.
Chanzo cha habari : Ofisi ya
Mwasilisno ya Waziri Mkuu.Endelea kuhabarika na P5 TANZANIA.
Comments