MATUKIO YA WIKI MKOANI KATAVI NA TANZANIA KWA UJUMLA KUANZIA JANUARI 18-23,2016.
Tuesday,
19 January 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Tuesday, January
19, 2016
Na.Issack Gerald-MPANDA
VIJANA
watatu wakazi wa Mpanda mjini jana wamefikishwa katika mahakama ya Mwanzo mjini
Mpanda, wakikabiliwa na shtaka la shambulio la kudhuru mwili.
Akisoma
shtaka hilo Mbele ya hakimu David Mbembela, koplo Mtei kutoka jeshi la polisi
Mpanda amewataja waliotenda kosa hilo kuwa ni Ramadhan Hamis mkazi wa Nsemulwa,
Maneno Shaban mkazi wa Mikocheni na Mohamed Mussa ambapo wote kwa pamoja mnamo
tarehe 14 Mwezi huu katika maeneo ya majengo mjini Mpanda, walimshambulia
Abdallah Salum mkazi wa Misunkumilo na kumsababishia maumivu makali.
Koplo
Mtei ameiambia mahakama kuwa mlalamikaji hakufika mahakamani kutokana na
kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Mpanda anakoendelea na matibabu kutokana
na kipigo alichopigwa na washtakiwa hao.
Aidha,
ameiomba mahakama hiyo isiruhusu dhamana kwa washtakiwa hadi pale taarifa
kuhusu hali ya muhanga zitakapotolewa.
Washtakiwa
wote wamekana shtaka na hakimu Mbembela amesema kutokana na ombi kutoka kwa
askari ambaye ni afisa wa serikali na amekula kiapo cha kusema ukweli, hivyo
mahakama imeridhia hoja iliyotolewa.
Kesi
hiyo itatajwa tena tarehe 22 mwezi huu na washtakiwa wamerudishwa rumande.
Tuesday,
19 January 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Tuesday, January
19, 2016
Na.Mwandishi wetu-DAR ES SALAAM
MKURUGENZI
Mtendaji Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Suleiman Lukanga,amesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuridhia na kutekeleza
uamuzi ulioisababishia serikali hasara na upotevu wa fedha.
Taarifa ya kusimamishwa kazi sambamba na Mkurugenzi Mtendaji
Manispaa ya Kigoma Bw.Boniface Nyambele imetangazwa jana na Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George Simbachawene katika
mkutano na waandishi wa habari baada ya tangazo kutolewa na Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais Tamisemi Rebecca Kwandu.
Kwa
upande wake Mkrugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Bw.Suleiman Lukanga
anayekabiliwa na tuhuma za ununuzi hewa wa gari la kusomba taka kwa Sh milioni
92.75 na ubadhirifu wa fedha za ujenzi wa skimu ya umwagiliaji ya Kakese, Sh
milioni 294.
Naye
Mkurugenzi Boniface Nyambele wa manispaa ya Kigoma anayekabiliwa na tuhuma za uuzaji
wa nyumba za halmashauri bila kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo,
zinazomtaka awe na kibali cha waziri mwenye dhamana.
Nafasi
ya Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda itakaimiwa na Lauteri Kanoni ambaye
ni Katibu Tawala Msaidizi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku nafasi ya
Mkurugenzi Manispaa ya Kigoma ikikaimiwa na Sultan Ndilowa ambaye ni Mkuu wa
Idara ya Maji Manispaa ya Kigoma
Aidha,Waziri
Simbachawene amewataka wakurugenzi watendaji wa mamlaka za serikali za mitaa
nchini kuwa makini katika kutekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria, kanuni na
taratibu zilizopo.
Amesema
serikali haitasita kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wote,ambao
watakiuka matakwa ya sheria, kanuni na taratibu na kutoweka mbele maslahi ya
umma.
Tuesday,
19 January 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Tuesday, January
19, 2016
Na.Boniface
Mpagape-Mpanda
MTU
mmoja mmoja mkazi wa Kasokola wilayani Mpanda Bw. Godfrey Kipyela, jana
amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo mjini Mpanda akikabiliwa na shtaka la
kudhuru mwili.
Akisoma
shtaka hilo, KIoplo Mtei wa jeshi la polisi Mpanda amesema mshtakiwa alitenda
kosa hilo tarehe 13 desemba mwaka 2015, saa moja usiku maeneo ya Kasokola
ambapo alimshambulia Bi. Maria January kwa kumpiga ngumi maeneo mbali mbali ya
mwili na kumsababishia maumivu makali.
Hakimu
wa mahakama ya Mwanzo mjini Mpanda Bw. David Mbembela baada ya kusikiliza
maelezo ya mlalamikaji pamoja na ushahidi uliotolewa na mtoto mdogo mwenye
umria wa miaka sita, amesema mlalamikaji anapaswa kuwasilisha mahakamani hati
ya matibabu yenye muhuri kutoka hospitali alikopatiwa matibabu.
Kesi
hiyo itasikilizwa tarehe 21 mwezi huu, na dhamana dhidi ya mshtakiwa
inaendelea.
Posted By:Issack Gerald | At:Monday, January
18, 2016
Na.Issack Gerald-MPANDA
HALMASHAURI
zote zilizomo ndani ya mkoa wa katavi zimetakiwa kufanya jitihada za
kutatua changamoto za miundombinu ya
elimu ili kuhakikisha wanafunzi wote wanasoma vizuri.
Hayo yamesemwa na Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Katavi Bw.Said Mwapongo wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA ofisini kwake kwa njia ya simu.
Hayo yamesemwa na Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Katavi Bw.Said Mwapongo wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA ofisini kwake kwa njia ya simu.
Amesema tayari ngazi ya mkoa imekutana na
ngazi za halmashauri lengo likiwa ni kuangalia utatuzi wa changamoto hizo kutokana na ongezeko la wanafunzi katika
sule mbalimbali.
Aidha Bw mwapongo
ameitaka jamii kuwapeleka watoto shule bila kisigizio chochote cha kutokuwa na sare ya shule na kuwa kwa mzazi au mlezi atakosa sare ya
shule ampeleke atapokelewa huku jitihada
za kutafuta sare zikiendelea kufanyika.
Mkoa
wa Katavi unaundwa na Halmshauri 5 ambazo ni Halmshauri ya Wilaya ya
Mpanda,Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda,Halmashauri ya Wilaya ya
Nsimbo,Halmshauri ya Wilaya ya Mlele na Halmshauri ya Wilaya ya Mpimbwe
Tuesday, 19 January 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Tuesday, January
19, 2016
Na.Issack Gerald-Katavi
Mkoa
wa Katavi umepokea Zaidi ya Shilingi Milioni 80 kwa ajili ya kugharimia mpango
wa serikali wa elimu bure kwa wanafunzi kuanzia Chekechea hadi kidato cha nne.
Kaimu
Afisa elimu Sekondari Mwalimu Said
Mwapongo amesema kuwa Mkoa wa Katavi umepokea zaidi ya milioni 80 na tayari
zimesambazwa katika shule kwa ajili ya matumizi yaliyokusudiwa.
Afisa
elimu Mwapongo,pamoja na kutoa wito kwa jamii,anatolea ufafanuzi wa michango
hiyo ambayo imefutwa pamoja na ile inayopaswa kuchangwa.
Kuhusu
wanafunzi waishio shule za bweni ambazo ni za Kata,Mwapongo amesema kuwa ziko
kwenye mpango wa serikali wa kuziondolea michango inayotoka kwa wazazi kutokana
na mpango wa wanafunzi waishio bweni kuwa katika mipango ya wazazi,walimu na
bodi za shule.
Ufafanuzi
huo wa Kaimu Afisa Elimu umekuja kufuatia malalamiko ya baadhi ya wazazi
wakihoji kulikoni wanafunzi waendelee kuchangishwa michango ya vitu mbalimbali
kama vyakula,pesa ya mlinzi na mpishi.
Mmoja
wa wakazi kutoka kijiji cha Kabulonge Kata ya Litapunga Wilayani Nsimbo ambaye
hakutaka jina lake litajweanasema yeye amekuwa na maswali mengi baada ya mtoto
wake aliyeko katika Shule ya sekondari machimboni kuanmbiwa atoe michango
wakati mtoto wake akipelekwa kuanza kidato cha kwanza.
Hata
hivyo baadhi ya wazazi,walezi na jamii kwa ujumla imeonekana kutoelewa vizuri
mchanganuo wa michango iliyofutwa na ilea ambayo jamii inapaswa kuendelea
kuchagia.
Kwa
Upande wake Afsisa elimu Sekondari Manispaa ya Mpanda Bi.Enelia Lutungulu
amesema kuwa kesho wanatarajia kukutana na bodi za elimu kwa shule zilizo
katika kata za Magamba,Kasokola na Shanwe kwa ajili kuweka sawa mazingira ya
utekelezaji wa sera ya elimu bure.
Katika
fedha hiyo Wilaya ya Mlele imepata zaidi ya Shilingi Milioni 32 kwa ajili ya
elimu za msingi na sekondari na huku
hesabu ya kujua kiasi kilichopokewa kwa upande wa Wilaya ya Mpanda na Nsimbo
kikiendelea kuchanganuliwa vizuri.
Idara
ya elimu sekondari Mkoa wa Katavi kwa Ujumla imesema kuwa,wanaendelea kuweka
mikakati ili kuhakikisha wanashika nafasi ya juu katika mithani ya taifa kwa
ngazi ya shule za sekondari kama ilivyo kwa shule za Msingi ambapo Mkoa wa
Katavi umeshika nafasi ya kwanza kwa mwaka 2015 huku Manispaa ya Mpanda
ikishika nafasi ya kwanza kitaifa kwa miaka 2 mfululizo yaani mwaka 2014 na
2015.
Kwa
mjibu wa barua ya tarehe 23 Novemba mwaka 2015 iliyoandikwa na Wizara ya Elimu
na mafunzo ya ufundi na kusambazwa katika shule zote hususani za Sekondari
Tanzania bara,inamtaka kila Mkuu wa shule kumpatia mwanafunzi fomu iliyotolewa
na Wizara na siyo ile iliyokuwa ikiandaliwa na bodi au kamati za shule na lengo
kuu likiwa kuondoa migogoro ya michango ya shule moja kutofautiana na shule
nyingine Wakati huo huo barua ya Novemba 27 mwaka 2015 ikiainisha wajibu wa
mzazi,mlezi,mwalimu,bodi au kamati za shule na jamii kwa ujumla.
Tuesday,
19 January 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Tuesday, January
19, 2016
Issack
Gerald-DAR ES SALAAM
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema,Serikali imepanga kufungua viwanda vya kusindika
ngozi kwenye mikoa ya Shinyanga, Geita na Dar es Salaam ili kutoa soko kwa
ngozi za wanyama wanaochinjwa kwenye machinjio ya mikoa hiyo.
Majaliwa ametoa kauli hiyo jana jioni wakati akizungumza na
baadhi ya Watanzania waishio Botswana kwenye kikao kilichofanyika kwenye kituo
cha mikutano ya kimataifa (GICC), jijini Gaborone, Botswana.
Waziri Mkuu amekuwa nchini Botswana
kwa ziara ya siku moja kumwakilisha Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano
wa SADC Double Troika yaani kikao maalum cha Wakuu wa Nchi na Serikali na Wakuu
wa Nchi wanaounda Chombo cha Ushirikiano wa Siasa,Ulinzi na Usalama.
Amesema Serikali imeamua kuongeza
viwanda nchini, kama njia mojawapo ya kukuza uchumi,kuacha kuuza mali ghafi
lakini pia ni fursa ya kuongeza ajira kwa Watanzania.
Wakati huo huo akijibu hoja
zilizoainishwa kwenye risala yao, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali bado
ina nia ya kuhamia Dodoma na kwamba itaendelea kutenga fedha zaidi ili wizara
nyingi zijenge ofisi zao Dodoma.
Aidha Waziri Mkuu Majaliwa ametumia
fursa hiyo kuwataka Watanzania waishio ughaibuni kutafuta fedha za mitaji
ambapo fedha hizo zinaweza kuwa zao au kupitia kwa marafiki zao ili waweze
kuwekeza nyumbani Tanzania.
Awali akisoma risala yao kwa niaba ya
wenzake, Mwenyekiti wa Chama cha Watanzania waishio nchini Botswana Bw. Neiman
Kissasi amesema chama hicho kilianzishwa mwaka 1992 kikiwa na lengo la
kuwaunganisha Watanzania waishio Botswana pamoja kujenga undugu wao na kusaidiana.
Katika risala yao, wameshauri
wafugaji wa Tanzania waelimishwe na kuwezeshwa kufuga kisasa na kuondokana na
ufugaji wa kurandaranda.
Vilevile, wameiomba Serikali ifungue
fursa za kiuchumi kwenye mikoa mingine ya Tanga, Lindi, Mtwara, Pwani, Kigoma,
Mbeya, Mwanza na Arusha badala ya kuziacha ziwe Dar es Salaam peke yake.
Waziri Mkuu amerejea jijini Dar es
Salaam jana usiku.
Chanzo
cha habari : Ofisi ya Waziri Mkuu
Tuesday, 19 January 2016
WATATU KATA YA MPANDA NDOGO WAFIKISHWA MAHAKAMANI MPANDA
WAKITUHUMIWA KUJIPATIA SHILINGI MIL.3,400,000/= KWA NJIA YA UDANGANYIFU
Posted By:Issack Gerald | At:Tuesday, January
19, 2016
Na.Issack
Gerald-Mpanda
WATU
wawili wakazi wa kata ya Mpanda ndogo wilayani Mpanda mkoani Katavi, jana
wamefikishwa katika mahakama ya mwanzo mjini Mpanda wakikabiliwa na shtaka la
kujipatia fedha shilingi milioni tatu na laki nne kwa njia ya udanganyifu.
Mlalamikaji
Bw. Lyango Joseph Mkazi wa Katumba ameiambia mahakama hiyo kuwa washtakiwa
Mustafa Mfaume na Mohamed Salum walitenda kosa hilo la kujipatia fedha kwa njia
ya udanganyifu kati ya mwaka 2014 na 2015.
Mbele
ya hakimu wa mahakama hiyo Bw. David Mbembela, mlalamikaji Bw. Lyango Joseph
amesema kuwa, mshtakiwa namba moja ambaye ni Bw. Mustaph Mfaume mnamo tarehe 20
mwezi desemba mwaka 2014 alienda nyumbani kwa Lyango Joseph na kuomba shilingi
laki nne kwa lengo la lengo la kufanyia shughuli za kilimo cha tumbaku katika maeneo
ya Kapemba kwa ahadi kuwa akiuza tumbaku atarudisha fedha alizokopa bila riba.
Mlalamikaji
Bw. Lyango Joseph ameiambia mahakama hiyo kuwa mnamo tarehe 16 mwezi januari
mwaka 2015 mshtakiwa namba moja aliongeza tena ombi la kukopeshwa shilingi laki
nne kwa lengo lile lile. Amesema mnamo tarehe 05 mwezi februari mwaka 2015
aliomba akopeshwe tena shilingi laki tatu kwa ahadi ya kurejesha atakapouza
tumbaku.
Mlalamikaji
ameendelea kuiiambia mahakama ya mwanzo mjini Mpanda kuwa, mnamo tarehe 23
mwezi April mwaka 2015 mshtakiwa Mustafa Mfaume, aliomba tna akopeshwe shilingi
laki sita lwa lengo lile lile la kuendeleza kilimo cha zao la tumbaku.
Bw.
Lyango amesema mwezi April mwishoni tarehe ambayo mlalamikaji haikumbuki,
mshtakiwa namba moja Bw. Mustafa Mfaume alikwenda tena nyumbani kwa mlalamikaji
Kanoge ambaye ni rafiki yake wa muda mrefu na kuomba tena shilingi laki mbili
ili aendeshee kilimo cha tumbaku na alikopeshwa fedha hizo na mwishoni mwa
mwezi Mei tarehe ambayo mlalamikaji haikumbuki mshtakiwa namba moja Bw. Mustafa
Mfaume alimpeleka mshtakiwa namba mbili Bw. Mohamed Salum na kuomba amdhamini apewe shilingi laki mbili
lakini mlalamikaji Bw. Lyango Joseph alikataa kwa kuwa hamfahamu na ndipo
Mshtakiwa Mustafa Mfaume akadai anamdhamini, na kutokana na ukaribu na urafiki
wao alikubali na kumkopesha kiasi hicho cha fedha.
Mlalamikaji
amesema kwa mara ya mwisho mshtakiwa Mustafa Mfaume alikwenda kwake tarehe 12
mwezi Mei na aliomba fedha shilingi milioni moja na laki mbili ili zitumike
kwenye shamba lake la tumbaku na kuahidi atakapouza na kupata malipo atarejesha
fedha hizo bila riba.
Mlalamikaji
Bw. Lyango Joseph amesema mshtakiwa namba moja Bw. Mustafa mfaume alikuwa
amejipatia jumla ya shilingi milioni tatu na laki mbili na mshtakiwa namba
mbili Bw. Mohamed Salum alijipatia shilingi laki mbili na kufanya jumla kuu ya
fedha walizojipatia kwa udanganyifu kuwa shilingi milioni tatu na laki nne.
Awali
washtakiwa wote wawili walitiwa hatiani na mahakama hiyo na kuhukumiwa kifungo
cha miezi sita jela kutokana na kukiri kosa la kujipatia pesa kwa njia ya
udanganyifu toka kwa Bw. Lyango Joseph na hukumu hiyo iliwataka watakapomaliza
kutumikia adhabu ya kifungo jela, warejeshe fedha kwa mlalamikaji lakini baada
ya kutoka jela hawakutekeleza amri ya
mahakama ya kumlipa mlalamikaji.
Mlalamikaji
katika shauri hilo Bw. Lyango Joseph ametoa pia vielelezo vya hati 6
walizoandikiana pamoja na nakala ya uamuzi wa mahakama uliowatia hatiani
washtakiwa. Washtakiwa wamekubali vielelezo vyote vilivyotolewa mbele ya
mahakama ya mwanzo mjini Mpanda.
Hakimu
wa mahakama hiyo Bw. David Mbembela amesema kwa kuwa washtakiwa hawajapinga
nakala ya uamuzi wa mahakama iliyowatia hatiani, hata hivyo hati 6 zilizotolewa
mahakamani kama kielelezo mahakama imezikataa mpaka zithibitishwe na kamishna
wa viapo ili ziweze kutambulika kisheria kuwa ni hati halali.
Kesi
hiyo imeahirishwa hadi tarehe 03 mwezi Februari mwaka huu, kungoja ushahidi
kutoka kwa washauri wa mahakama waliosikiliza kesi hiyo tangu mwanzo ambapo
hata hivyo hamimu Mbembela amesema dhamana kwa washtakiwa zinaendelea.
Wednesday,
20 January 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday,
January 20, 2016
Na.Issack Gerald-Katavi
Watu
wawili waliofahamika kwa majina ya Kupiwa Julius (28) na Lemmy Madirisha wote
wakazi wa Mkazi wa Ilebura wamepigwa na radi na kufariki dunia papo hapo.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Katavi Dhairi Kidavashari amesema kuwa tukio hilo limetokea
jana majira ya saa nane na nusu mchana katika kijiji cha Ilebura Tarafa ya
Kabungu Wilaya ya Mpanda.
Amesema
kuwa,katika tukio hilo,watu watatu waliojeruhiwa wametajwa kuwa ni Tatu Gerald
(28),Stela John (38) na Philbert Paschal wote wakazi wa kijiji cha Ilebura.
Aidha
kamanda Kidavashari amesema,kabla ya tukio marehemu na majeruhi kwa pamoja
walikuwa shambani wakilima ambapo wakati wakiendelea kulima mvua ilianza
kunyesha ambapo wote waliamua kwenda chini ya mti kujikinga na mvua na ndipo
radi ilipopiga na kupelekea madhara hayo.
Ameongeza
kuwa baada ya tukio hilo majeruhi wote wamepelekwa katika hospitali ya Wilaya
ya Mpanda na wanaendelea na matibabu huku miili ya marehemu ikiwa imekabidhiwa
kwa ndugu zao kwa ajili ya mazishi.
Hata hivyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi
anawatahadharisha wananchi wote kuwa makini katika kipindi hiki cha masika
pindi mvua zinaponyesha kwa kujihifadhi maeneo salama ilikuepukana na madhara
kama haya ambayo huadhiri ustawi wa afya na uhai wa watu.
Wednesday,
20 January 2016
WANAOGOMBANIA ARDHI NSIMBO WATAKIWA KUTOKA,ELIMU BURE BADO
KUELEWEKA IPASAVYO KWA WANANCHI MKUU WA WILAYA YA MLELE ATOA NENO
Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday,
January 20, 2016
Na.Agness Mnubi-Nsimbo.
WADAU
wa Elimu katika halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi wametakiwa
kuelimisha wazazi na walezi juu ya Mfumo wa elimu bure.
Wito
huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Mstaafu Issa Suleiman Njiku
katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika jana katika Halmashauri ya
Wilaya ya Nsimbo, mara baada ya madiwani wa halmashauri hiyo kuhoji juu ya
Mfumo wa elimu bure.
Amefafanua
kuwa ni wajibu wa Mkurugenzi kuitisha kikao cha wadau wa elimu ili kuwaelimisha
wazazi na walezi juu ya Mfumo wa elimu
bure.
Aidha
amesema taarifa juu ya elimu bure
zibandikwe kwenye mbao za matangazo, ili kurahisisha kusambaza elimu hiyo na
kuwataka madiwani wa halmashauri ya Nsimbo kutoa taarifa za walimu wanaotoza
ada na mahitaji mengine ya wanafunzi ambayo yanagharimiwa na serikali.
Wakati
huo huo,idara ya Maliasili na Misitu katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo
imeagizwa kutatua mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa kata ya Urwila na kata
ya Katumba, kuhusu kilimo katika eneo la Nzaga ambalo ni chanzo cha mto.
Kanali
Njiku ameongeza kuwa,wananchi wa Vijiji hivyo wanagombania kulima katika mpaka
wa eneo la mto, kinyume cha sheria na kufafanua kuwa sheria inaelekeza shughuli
za kibinadamu kuanza umbali wa mita 60 kutoka chanzo cha maji.
Kufuati
hali hiyo, amewataka wananchi wanaoishi katika misitu na hifadhi ya serikali,
kuhama na kuacha tabia ya kukata misitu na kuendesha shughuli yoyote katika
hifadhi za serikali.
Wednesday,
20 January 2016
AMPA UJAUZITO DADA YAKE WA MIAKA 14 SUMBAWANGA POLISI
WAMDAKA,IDARA YA ELIMU NAKO KALAMBO HARAKATI KWA KWENDA MBELE
Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday,
January 20, 2016
Na.Issack Gerald-Sumbawanga
POLISI wilayani
Sumbawanga Mkoani Rukwa inamshikilia mkazi wa kijiji cha Ulinji, Manispaa ya
Sumbawanga mwenye umri wa miaka 28 kwa tuhuma za kumpa ujauzito dada yake mwenye
umri wa miaka 14 anayesoma darasa la saba.
Inadaiwa kuwa
mtuhumiwa ambaye amemtaliki mkewe, alirejea kuishi nyumbani kwa wazazi wake
kijijini Ulinji miaka miwili iliyopita kabla ya kumpatia ujauzito mtoto huyo wa
baba yake mkubwa.
Polisi
imethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kwamba alikamatwa na Ofisa
Mtendaji wa Kijiji cha Ulinji, Manispaa ya Sumbawanga, Linus Mbutu.
Ofisa Mtendaji
wa Kijiji cha Ulinji, amesema mtuhumiwa amekamatwa juzi na askari wa Mgambo wa
kijiji hicho akiwa amejificha kwa saa tatu porini akikwepa kukamatwa.
Katika hatua nyingine,idara ya elimu
wilayani Kalambo mkoani Rukwa jana
imefanya kikao cha kujadili upungufu wa madawati uliopo wilayani humo.
Akizungumza na P5
TANZANIA MEDIA sambamba na mpanda radio kwa njia ya simu afisa elimu vifaa
na takwimu wa halmashauri ya wilaya ya Kalambo
Bi. Toba Mwihanga ameziomba
taasisi mbalimbali kutoa msaada ili kutatua changamoto hiyo.
Bi. Mwihanga amesema mwaka 2014
walipokea madawati 100 ambayo hayakukidhi mahitaji ya wanafunzi.
Aidha ameitaka jamii kuendelea
kushiriki katika ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu na vyoo,huku akiwataka
watendaji wa kata kuhamasisha jamii juu ya elimu bure , na kuiomba serikali
kuongeza walimu katika mkoa huo.
Wednesday,
20 January 2016
WAKAZI KATAVI WATAKIWA KUWA MAKINI NA MVUA KUEPUKA MAFURIKO
PIA IDARA ZA MAAFA KATIKA HALMSHAURI ZOTE ZAAGIZWA KUJIPANGA KIKAMILIFU
Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday,
January 20, 2016
Na.Boniface Mpagape-Mpanda
MKUU
wa Mkoa wa katavi Dk. Ibrahim Msengi amewataka wakazi wa mkoa huo,kuchukua
tahadhari kutokana na uwezekano wa kuwepo kwa mafuriko kama ilivyotabiriwa na
wataalam wa hali ya hewa.
Mkuu
wa mkoa wa Katavi ametoa tahadhari hiyo wakati akizungumza na Mpanda radio
ofisini kwake sambamba na P5 TANZANIA
MEDIA.
Amesema
wakazi wa mkoa wa Katavi wamekuwa wakijenga katika maeneo ambayo hayaruhusiwi
kwa makazi na kuwataka wawe katika maeneo yasiyo hatarishi.
Amewaagiza
wakurugenzi, na wakuu wa wilaya zote mkoani Katavi kwa kushirikiana na kamati zao za maafa
kujiandaa kikamilifu kwa kutoa tahadhari kwa wananchi ili kukabiliana na maafa
yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua za El-Nino.
Thursday,
21 January 2016
WANAFUNZI WANYESHEWA MVUA WAKISOMEA CHINI YA MIEMBE WILAYANI
MPANDA,WAZAZI WAISHIWA NGUVU WAIOMBA SERIKALI KUSAIDIA
Posted By:Issack Gerald | At:Thursday,
January 21, 2016
Na.Issack
Gerald-Mpanda
Wazazi
wa wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Msingi Sambwe iliyopo mtaa wa
Kampuni Kata ya Misunkumilo Manispaa ya
Mpanda,wameiomba serikali kuwasaidia kumalizia ujenzi wa madarasa katika shule
hiyo ili wanafunzi hao waondokane na adhaa ya kunyeshewa na mvua inayoambatana na radi wakiwa chini ya miembe.
Hayo yamebainishwa na wazazi hao wakati wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Sambamba na Mpanda
Radio Katika mtaa huo,kuhusu namna wazazi wanavyojitolea katika ujenzi wa
madarasa shuleni hapo.
Aidha
wamesema kuwa,baadhi ya watoto wamekuwa wakiugua magonjwa kama homa,maralia na
mengineyo huku daftari zikilowana kutokana na wanafunzi kukosa mahala pa
kujisitiri.
Baadhi
ya Wazazi waliozungumza ni pamoja na Mussa Daudi,Huruma Washega na Peter Paul
Masesela wote wakazi wa Mtaa wa Kmpuni ambao pia wamesema kutokana na kuishiwa
pesa hawana namna zaidi ya kuitegemea serikali kutokana na uwezo wao kufikia
kikomo.
Hata
hivyo wameeleza kusikitishwa na serikali kuwafukuza wachimbaji wadogowadogo
katika mgodi wa Kampuni ambapo wachimbaji hao kila mara wamekuwa sehemu
mojawapo ya chanzo cha Mapato katika kuendesha maendeleo ya shule.
Katika
hatua nyingine,wameiomba serikali kumuweka
katika mfumo wa malipo mwalimu Alex Sangu ambaye amekuwa akifundisha
katika shule ya Sambwe kwa muda mrefu ikizingatiwa kuwa hawana tena uwezo wa
kulipa kutokana na kipato chao kidogo kinachotosheleza kuendesha familia zao.
Hata
hivyo Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bw.Charles Kassian ,hakuwa tayari kuzungumza
na P5 TANZANIA MEDIA sambamba na Mpanda Radio kuhusu maendeleo na hali ya shule
zaidi ya kusema kuwa labda atazungumza baada ya mwezi mmoja kuanzia sasa.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Kampuni Bw.James Simon amekiri wanafunzi
kusomea chini ya miembe tangu shule zifunguliwe
Januari 11 mwaka huu ukizingatia kuwa ni msimu wa mvua za masika
zinazoambatana na radi.
Hata
hivyo Bw.Simoni,amewataka wananchi kuendelea kuwa wavumilivu wakati masuala
mbalimbali yakiwemo kumlipa mwalimu wakati yakifanyiwa kazi ambapo wakati huo
huo amesema kuwa siku ya jumatano ya wiki ijayo wanatarajia kuitisha mkutano wa
hadhara kujadili maendeleo ya shule.
Shule
ya Msingi Sambwe,ina walimu 2 walioajiriwa na seriklai huku mmoja akiwa ni wa
kujitolea ambo shule hiyo iliyosajiriwa mwaka huu ina wanafunzi wapatao 150
kuanzia darasa la kwanza hadi la nne.
Hata hivyo Meya wa Manispaa ya Mpanda Bw. Philipo Mbogo ambaye ni miongoni mwa walioanzisha shule hiyo baada ya kuona kuwa watoto wanahangaika kwenda kusomea umbali mrefu,ameiambia P5 TANZANIA MEDIA na Mpanda Radio Kuwa suala la shule hii linafahamika na linafanyiwa kazi.
Siku ya jana,kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari,alitoa wito kwa wakazi Mkoani Katavi kujikinga na mvua sehemu iliyo salama ikiwa ni pamoja na kueupa kwenda chini ya miti ambapokwa kiasi wanafunzi hawa hawatofauriani na mazingira kama hayo kwa kuwa hakuna madarasa.
Hata hivyo Meya wa Manispaa ya Mpanda Bw. Philipo Mbogo ambaye ni miongoni mwa walioanzisha shule hiyo baada ya kuona kuwa watoto wanahangaika kwenda kusomea umbali mrefu,ameiambia P5 TANZANIA MEDIA na Mpanda Radio Kuwa suala la shule hii linafahamika na linafanyiwa kazi.
Siku ya jana,kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari,alitoa wito kwa wakazi Mkoani Katavi kujikinga na mvua sehemu iliyo salama ikiwa ni pamoja na kueupa kwenda chini ya miti ambapokwa kiasi wanafunzi hawa hawatofauriani na mazingira kama hayo kwa kuwa hakuna madarasa.
Thursday, 21 January 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Thursday,
January 21, 2016
Na.Issack
Gerald-Mpanda
Wachimbaji wadogowadogo wa dhahabu katika mgodi wa
Kampuni Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamesikitishwa na kitendo cha serikali
kuwapiga marufuku uchimbaji wa madini katika mgodi huo kwa madai kuwa eneo hilo
ni miliki ya makambi ya jeshi.
Hayo
yamebainishwa na wachimbaji hao wakati wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Sambamba na Mpanda Radio mgodini hapo kuhusu namna wanavyoathirika
kutokana na kufukuzwa katika mgodi huo.
Wamesema
kuwa wanategemea mgodi huo kuendesha maisha ya kila siku ikiwemo kusomesha
watoto na kulipia kodi ya nyumba.
Mwenyekiti
wa mtaa wa Kampuni Bw.Simon James amesema kuwa,kufukuzwa kwa wachimbaji hao
wapatao 200 kumepelekea vitendo vya wizi kuibuka ambapo jana mifugo ikiwemo
nguruwe na mbuzi kadhaa wameibwa katika makazi ya watu.
Kwa
mjibu wa maelezo ya wajimbaji hao walioanza kuchimba eneo hilo miaka ya 1980
wamesema kuwa wanategemea kuendesha maisha kutokana na mgodi huo.
Baadhi
ya wachimbaji wadogo ambao wamezungumzia khusu wanavyoathiliwa na kufukuzwa
katika mgodi huo ni pamoja na Athman Omary,Lucas Juma,Nuru Hassan na Faustin
Method Kamatasimba
Kwa
upande wake Mjumbe wa seriklai ya Mtaa wa Kampuni Bi.Flora Simon Mpenda,amesema
kuwa kufukuzwa kwa wachimbaji hao kumeathiri mapato ya kuendesha shule ya
Msingi Sambwe.
Kwa
upande wake Meya wa Manispaa ya Mpanda Bw.Wilium Philipo Mbogo amesema kuwa
suala hili lipo katika mamlaka husika kwa mazungumzo ili lipatiwe
ufumbuzi.
Wiki iliyopita,madiwani wa balaza la Manispaa ya Mpanda kupitia kikao chake cha januari 14 mwaka huu waliiomba Manispaa ya Mpanda kuweka mipaka kati ya eneo la jeshi na makazi ya raia ili kuondoa migogoro ya ardhi.
Wiki iliyopita,madiwani wa balaza la Manispaa ya Mpanda kupitia kikao chake cha januari 14 mwaka huu waliiomba Manispaa ya Mpanda kuweka mipaka kati ya eneo la jeshi na makazi ya raia ili kuondoa migogoro ya ardhi.
Thursday,
21 January 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Thursday,
January 21, 2016
Na.Boniface Mpagape:Mpanda
SERIKALI
Mkoani katavi inatarajia kutoa semina kwa viongozi wa serikali kuanzia ngazi za
vijiji, kata na tarafa ili watambue vyema majukumu yao.
Mkuu
wa mkoa wa katavi Dk. Ibrahim Msengi amesema hayo wakati akizungumza na P5
TANZANIA MEDIA Sambamba na Mpanda radio ofisini kwake. Amesema imebainika kuwa
baadhi ya viongozi wa serikali katika ngazi hizo mkoani Katavi wamekuwa
hawatambui vizuri majukumu na mipaka ya madaraka waliyonayo.
Amesema
semina hiyo inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni itawajengea uwezo wa kutambua
uwajibikaji wao kwa wananchi na kurahisisha utendaji kazi.
Aidha
Mkuu wa mkoa wa Katavi amesema semina hiyo itakuwa ni chachu ya kuleta mabadiliko
katika ngazi za uongozi kwani wahusika watapaswa kutoa taarifa kuhusu utendaji
wao na itakuwa rahisi kupima uwajibikaji wao katika shughuli za maendeleo.
Thursday,
21 January 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Thursday,
January 21, 2016
Na.Vumilia Abel-Nsimbo
JAMII
wilayani Nsimbo mkoani katavi imeombwa kushiriki katika matengenezo madogo
madogo ya miundombinu ya barabara.
Ushauri
huo umetolewa na mkurugenzi wa
halmashauri ya Nsimbo Bw Michael Nzyungu wakati akizungumza na P5 TANZANIA sambamba na mpanda radio Ofisini
kwake.
Amesema,
hali ya
miundombinu ya barabara hairidhishi
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha
na kuwa baadhi hazikusajiliwa wala kutengewa bajeti, na zipo katika
mikakati ya kusajiliwa ili zipatiwe bajeti kwa mwaka wa fedha 2016 /2017.
Bw.
Nzyungu amezitaja baadhi ya barabara zilizotengewa bajeti ni
Itenka, Magamba, Kasalala, Sungamila, Katumba complex1 na Katumba complex B, Urwila na Usense.
Aidha,
amewataka madiwani na watendaji waonapo
dalili hatarishi ya kuharibika miundombimu hiyo watoe taarifa mapema ili hatua
zichukuliwe.
Thursday,
21 January 2016
MAAFISA ELIMU NSIMBO WAPEWA SIKU 6 KUHAKIKISHA WANAFUNZI
WALIOCHAGULIWA KUINGIA SEKONDARI WANARIPOTI
Posted By:Issack Gerald | At:Thursday, January
21, 2016
Na.Agness Mnubi-Nsimbo.
MAAFISA
elimu sekondari katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo wamepewa siku 6 kuanzia
jana, kuhakikisha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha
kwanza wanaripoti.
Akizungumza
juzi katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo,
Mkuu wa Wilaya ya Mlele kanali mstaafu Issa Suleiman Njiku, amesema mahudhurio
ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza si mazuri
na kuwataka maafisa elimu kushirikiana na wenyeviti na watendaji wa vitongoji,
vijiji na kata, kuhakikisha wanafunzi hao wanaripoti shuleni.
Aidha
Kanali Njiku ameutaka uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo kuhakikisha
unatekeleza tamko la Waziri wa TAMISEMI juu ya kutatua changamoto ya upungufu
wa madawati.
Amesema
mkoa wa Katavi umetoa muda hadi mwisho
wa mwezi Machi, kuhakikisha halmashauri zote zinatekeleza agizo hilo, na
halmashauri ambayo haitatekeza, Mkurugenzi atachukuliwa hatua za kisheria.
Thursday,
21 January 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Thursday,
January 21, 2016
Na.Issack Gerald-Katavi
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ndiyo kitovu cha
nchi na kwamba kila Mtanzania ameelekeza jicho lake pale kwa sababu anasubiri
kupata huduma ya msingi.
Ametoa kauli hiyo leo wakati
akizungumza na wakurugenzi, wakuu wa taasisi na watumishi wa Ofisi ya Rais -
TAMISEMI kwenye mkutano uliofanyika ofisi ya TAMISEMI mjini Dodoma.
Waziri Mkuu ameitaka ofisi hiyo
ihakikishe inaisimamia vizuri mikoa na halmashauri ili Serikali iweze kupata
matokeo mazuri na tarajiwa.
Waziri Mkuu alisema jukumu kubwa
lililopo hivi sasa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ni kuhakikisha kuwa
zinabuni vyanzo vipya vya mapato na kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato ya
serikali.
Alisema Serikali ya Awamu ya Tano
imekusudia kuwahudumia ipasavyo Watanzania wenye uelewa tofauti na matakwa
tofauti na kwa kuanzia Serikali imeanza kuwajenga watumishi wa Serikali
kutambua kuwa wao ni wahudumu wa wananchi hivyo inawapasa kuwahudumia vema.
Awali akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza
na watumishi hao, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Bw. George
Simbachawene alisema TAMISEMI wapo tayari kubadilika na kufanya kazi kama kauli
ya Rais John Pombe Magufuli inavyotaka, yaani HAPA KAZI TU.
Naye, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Bw. Bernard Makali alimpongeza Waziri Mkuu Majaliwa kwa kusimamia vizuri
masuala ya elimu nchini wakati akiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI anayeshughulikia
masuala ya elimu.
Friday,
22 January 2016
WANAFUNZI 1137 WILAYANI NKASI WATOKOMEA KUSIKOJULIKANA,AFISA
ELIMU KUTANGAZA MSAKO NYUMBA KWA NYUMBA.
Posted By:Issack Gerald | At:Friday, January
22, 2016
Na.Issack Gerald-Nkasi.
WANAFUNZI wapatao 1137 kati ya
2257 hawajaripoti shule kuanza kidato
cha kwanza mwaka huu katika Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa licha ya serikali
kutoa elimu bure.
Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA sambamba na
Mpanda Radio kwa njia ya mawasiliano ya simu Kaimu Afisa Elimu
sekondari Wilayani Nkasi Bw. Fortunatus Kaguo amesema kuwa,jumla ya
wanafunzi 2257 walichaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka huu lakini
hadi sasa walioripoti shuleni ni wanafunzi 1120 pekee huku wengine1137 wakiwa
hawajulikani walipo.
Aidha Afisa elimu huyo amewataka
wazazi kuwapeleka watoto wao shule na
atakayekaidi atachukuliwa hatua kali za
sheria.
Amefafanua kuwa wanamikakati ya
kuanzisha oparesheni ya nyumba kwa nyumba ili kuwasaka wazazi ambao
hawajawapeleka watoto wao shule.
Hatua ya kukosekana kwa wanafunzi hawa
kunafuatia ikiwa ni muda mfupi baada ya
Seriklai kutangaza mpango mkakati wa elimu bure kwa wanafunzi kuanzia Chekechea
hadi sekondari kwa wanafunzi wa kidato cha nne.
Friday,
22 January 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Friday, January
22, 2016
Na.Boniface Mpagape-Mpanda
TAASISI
ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Katavi, imemfikisha katika mahakama ya
wilaya ya Mpanda Afisa mtendaji wa mtaa
wa Kawajense akikabiliwa na shtaka la kushawishi na kupokea rushwa ya shilingi
elfu thelathini.
Taarifa
ya TAKUKURU Mkoa wa Katavi kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na Kaimu mkuu
wa TAKUKURU Mkoani Katavi Bw. Christopher Nakua imesema kuwa afisa mtendaji
huyo Bi. Catherine Kipeta, mnamo Jumatatu ya tarehe 18 mwezi huu aliomba rushwa
ya shilingi elfu thelathini kutoka kwa mwananchi ili asimpeleke kwenye baraza
la kata kwa kosa la kufungua sehemu ya biashara,muda wa kufanya usafi.
Amesema
TAKUKURU Mkoa wa Katavi ilifanya uchunguzi wa awali na kuandaa mtego na
kumkamata mshtakiwa baada ya kupokea rushwa kutoka kwa mwananchi huyo.
Mshtakiwa
amefikishwa katika mahakama ya wilaya tarehe 19 mwezi huu na kusomewa mashtaka
mawili yanayomkabili ambayo ni kuomba rushwa ya shilingi elfu thelathini na
kosa la pili ni kupokea rushwa, kinyume na matakwa ya mwajiri wake na kifungu
cha 15 (1) (a) cha sheria ya kuzuia na
kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
TAKUKURU
mkoa wa Katavi inatoa wito kwa wananchi wote kujiepusha na vitendo vya rushwa
ambavyo husababisha kutopatikana kwa haki, kutowajibika kwa watumishi wa umma,
kwenda kinyume na maadili, kanuni na viapo vya utumishi, uvunjaji wa haki za
binadamu, wananchi kukosa imani na idara, taasisi, mashirika mbalimbali ya
serikali.
Aidha,Taasisi
ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Katavi imesema kila mwananchi ana
wajibu wa kutoa taarifa ya vitendo vya rushwa katika ofisi hiyo iliyopo Mpanda
mjini, au kupitia simu ya bure namba 113.
Wananchi
wanapaswa kutetea haki, kuzuia rushwa kwani rushwa ni adui wa haki, na penye
sheria pana haki, penye haki pana amani, penye amani pana maendeleo.
Friday,
22 January 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Friday, January
22, 2016
Na.Mwandishi wetu-Dar es salaam
Watanzania
wametakiwa kuacha ushabiki wa vyama vya siasa na badala yake wajikite kutatua
matatizo ya kitaifa.
Hayo
yamebainishwa leo na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Josefu Sinde Warioba katika
kongamamno la tafakuri ambalo limefanyika Katika ukumbi wa chuo kikuu cha Dar
es salaa wakijadili hoja mbalimbali ikiwemo uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015.
Jaji
Warioba amesema kuwa ni lazima kuondoa matatizo ya Rushwa,ukabila,udini huku
akiwataka watanzania kuchagua viongozi wanaoona matatizo ya kitaifa kuliko
kuchagua viongozi wanaojali masuala ya vyama vyao.
Hata
hivyo baadhi ya wajumbe wa kongamano hilo,waligusia mambo mbalimbali yakiwemo
yanayohusu siasa kipindi cha uchaguzi mwaka 2015,nafasi ya vyombo vya habari
katika uchaguzi wa mawaka 2015 katika kuripoti hali ya uchaguzi,majukumu ya
viongozi wa kitaifa kama rais,mawaziri ,tume ya taifa ya Uchaguzi na katiba ya
Tanzania.
Kuhusu
Katiba baadhi ya wajumbe wametaka katiba ya jaji Joseph Sinde Warioba iwe ndiyo
katiba itakayojadiliwa huku wakitaka tume ya taifa ya uchaguzi kuwa huru ili
kupata uchaguzi wa huru na haki katika kipindi cha uchaguzi.
Kongamano
hilo limeshirikisha wasomi na wahitimu mbalimbali wa chuo kikuu cha Dar es
Salaam ambapo mwenyekiti wa kongamano hilo alikuwa ni Jaji Joseph Sinde
Warioba.
Asante kwa kunifuatilia kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM,usisahau kumshirikisha
mwenzako naye ahabarike,Ni mtangazaji wako Issack Gerald Bathromeo
Comments