WANAWAKE WAISHI KWA MIGOGORO KATIKA NDOA KISA UCHAGUZI OKTOBA 25,2015
Na.Issack
Gerald-Mpanda
BAADHI
ya wanawake Mkoani Katavi wameiomba Serikali na wadau mbalimbali kuelimisha jamii kwa chaguzi zijazo ili kukomesha tabia
ya ukandamizaji unaofanywa na baadhi ya wanaume kwa kuwachagulia vyama vya
siasa wake zao.
Baadhi ya wanawake ambao wamezungumza na P5 TANZANIA(Picha na Issack Gerald) |
Wakizungumza
na P5 TANZANIA MEDIA wamesema,
katika kipindi cha uchaguzi wa mwaka 2015, walikabiliwa na changamoto za
kuchaguliwa vyama na waume zao pamoja na lugha za matusi kwa baadhi ya vijana
ambao waliwataka kuwa chama kimoja.
Wamesema
mpaka sasa baadhi ya wanawake wameachika na wengine kuishi katika migogoro ya
ndoa pamoja na chuki kati yao na baadhi ya vijana kutokana na tofauti za
itikadi ya vyama vya siasa.
Pamoja
na changamoto walizozipata wanawake hao pia wamepongeza uchaguzi huo kufanyika
kwa amani na utulivu.
Aidh
awamesema kuwa kutolewa kwa elimu ya uchaguzi kwa jamii kuwatambua wanawake
kuwa wana uwezo wa kuongoza kutatoa fursa ya kuongeza idadi ya wanawake katika
ngazi mbalimbali za maamuzi.
Comments