AFIKISHWA MAHAKAMANI MPANDA KWA TUHUMA ZA UHARIBIFU WA MALI,YUMO PIA ALIYETISHIA KUUWA KWA MANENO
Na.Boniface Mpagape-Mpanda
MTU
mmoja mkazi wa Kapalangeo-kazima katika manispaa ya Mpanda Bw. Joseph Saleh
kajunja amefikishwa katika mahakama ya mwanzo mjini Mpanda akikabiliwa na
shtaka la kuharibu mali.
Akisomewa
shtaka mbele ya hakimu Robert Nyando, mshtakiwa alitenda kosa hilo tarehe 26
mwezi huu katika eneo la soko kuu Mpanda mjini kwa kuvunja kioo cha bajaji
yenye namba za usajili T 810 AGF chenye thamani ya shilingi laki moja na elfu
themanini, mali ya Bw. Dalam Moshi. Mshtakiwa amekana shraka hilo.
Hakimu
wa mahakama hiyo Bw. Robert Nyando, amesema mshtakiwa ana haki ya kupata
dhamana ya ahadi ya shilingi laki mbili na elfu hamsini na mdhamini awe na
barua toka kwa mtendaji wa kijiji na kitambulisho.
Kesi
hiyo imeahirishwa hadi tarehe 8 mwezi Februari mwaka huu itakaposikilizwa.
Wakati
huo huo, miongoni mwa kesi zilizotajwa leo ni ya kutishia kuua kwa maneno
ambapo Mlalamikaji Bi. Agnes Elikana amefikisha shtaka hilo katika mahakama ya
mwanzo Mjini Mpanda, kwa kutishiwa kuuliwa kwa maneno na Maria Joseph mkazi wa
Kilimahewa.
Imeelezwa
mahakamani hapo kuwa mshtakiwa Maria joseph alitenda kosa hilo tarehe 12 mwezi
huu majira ya saa 11 jioni huko Kilimahewa kata ya Shanwe, kwa kumtishia Agnes
Elikana kwamba atampiga mpaka amuue.
Baada
ya kusomewa shtaka mshtakiwa amekana kosa na hakimu wa mahakama hiyo
aliyesikiliza kesi hiyo Bw. Sylivester makombe amesema dhamana ipo wazi kwa
mshtakiwa ya ahadi ya shilingi laki mbili na awe na kitambulisho. Mshtakiwa
amedhaminiwa na kesi hiyo itasikilizwa tarehe 05 mwezi Februari mwaka huu.
Comments