HALI YA USALAMA BURUNDI HUENDA IKACHUKUA SURA MPYA
Na.Issack Gerald-Katavi
Hali ya kisiasa nchini Burundi huenda
ikachukua sura mpya baada ya serikali na upinzani kutoafikiana juu ya
yatakayozungumzwa kwenye mkutano ili kutatua mzozo nchini humo.
Jaji Augustine Mahiga Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimatifa akiwa ni miongoni mwa viongozi wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki wanaoshuruhisha mgogoro wa kisiasa nchini Burundi |
Kwa mujibu wa msemaji wa CNARED Jeremie
Minani amesema kuona serikali ilikataa kuhudhulia mkutano ambao ungefanyika
Januari 6,2016 jijini Arusha kuwa hawakuafikiana juu ya taerehe hiyo ilikuwa ni
kisingizio.
Amesema wanapaswa kujadiliana juu ya mzozo wa
Burundi ili wasije kutumbukia kwenye vita,kuachiwa huru kwa wafungwa dhidi ya
maandamano,utumwaji wa wanajeshi wa AU na kuundwa kwa serikali ya mpito.
Kwa upande wa serikali,mshauri mkuu wa rais
Willy Nyamitwe amesema kuwa mzungumzo yanatakiwa kujikita zaidi kwenye utatuzi
wa mgogoro wa Burundi hasa utawala bora. Pia wanapaswa kushirikishwa warundi
wato waliopo nchini na nje ya nchi.
Ingawa serikali ililalamika kuhusiana na
kuhudhulia kwa wasiostahili kwenye mkutano uliofanyikia nchini Uganda Waziri wa
ulinzi na usalama wa Uganda Crispus Kiyoga ameweka wazi kwamba pande zote
zinapaswa kushiriki iwe ni serikali au upinzani bila kuegemea upande wowote.
Hata hivyo mwenyekiti wa Umoja wa Afrika
Nkosazana Zuma ameitaka Burundi kukubali ujio wa wanajeshi hao wa kulinda
usalama.
Itakumbukwa kuwa rais Pierre Nkurunziza
ametishia kupigana na wanajeshi wa AU endapo watakanyaga ardhinim kwake bila
ruhusa ya serikali ya Burindi.
Na. Bukuru Elias Daniel - Burundi
Comments