Posts

Showing posts from September, 2017

MANISPAA YA MPANDA YASHINDWA KUPELEKA WAZEE DODOMA-Septemba 30,2017

Image
Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi UMOJA wa wazee Mkoani Katavi umesema Manispaa ya Mpanda imeshindwa kuwezesha wazee ili kwenda kushiriki maadhimisho ya siku ya wazee duniani yanayofanyika kila ifikapo tarehe moja ya mwezi wa kumi.

RAIS WA ZANZIBAR AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI WA TAASISI-Septemba 30,2017

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein,amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

WAZEE MKOANI KATAVI WAOMBA SERIKALI IWATENGENEZEE MAZINGIRA RAFIKI KATIKA MASUALA YA MATIBABU-Septemba 29,2017

Na.Issack Gerald-Katavi UMOJA wa wazee Mkoani Katavi kimeiomba serikali kuendelea kutengeneza mazingira yatakayomwezesha mzee kupatiwa huduma za matibabu bila usumbufu.

VIBOKO MKOANI KATAVI WASABABISHA NDOA KUVUNJIKA PIA UHARIBIFU WA MAZAO SHAMBANI-Septemba 29,2017

Image
Mfano wa picha ya viboko vinavyopatikana mto sitalike mkoani katavi Na.Issack Gerald-Katavi WAKAZI wa kijiji cha Milala Kata ya Misunkumilo katika Manispaa ya Mpanda,wameilalamikia serikali kutochukua hatua dhidi ya viboko waliopo bwawa la Milala vinavyoharibu mazao shambani na kutishia uhai wa binadamu mara kwa mara.

WAKAZI KATA YA MPANDA HOTEL WAELEZEA KUFURAHISHWA NA HATUA YA KUTATUA TATIZO LA MAJI-Septemba 29,2017

Na.Issack Gerald-Katavi BAADHI ya wakazi wa kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda wameelezea kufurahishwa na hatua ya uchimbaji mitaro ya kupitisha mabomba kwa ajili ya kuleta huduma ya maji katika katika kata hiyo.

HALMASHAURI ZOTE MKOANI KATAVI ZATAKIWA KUANDAA VITAMBULISHO VYA WAZEE-Septemba 28,2017

Na.Issack Gerald-Katavi Halmashauri  zote Mkoani Katavi zimetakiwa kuandaa vitambulisho kwa wazee wote waliokidhi vigezo vya kupatiwa matibabu bure.

WANAFUNZI 417 WAKATISHA ELIMU WILAYANI MLELE-Septemba 27,2017

Na.Issack Gerald-Mlele Katavi ZAIDI ya wanafunzi 417 wa sekondari katika halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi wamekatisha masomo yao kwa kipindi cha kati ya mwaka 2014 na 2016 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mimba na utoro Hali hiyo imebainishwa na Afisa elimu idara ya Sekondari Bw.Sylivanus Raphael Kunambi ambapo amesema kuwepo changamoto ya wanafunzi kuikatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo utoro na mimba. Kunambi amesema kwa mwaka 2014 wanafunzi 108 sawa na asilimia 17.4 ya wanafunzi wote waliokuwa wamesajiliwa katika mwaka huo hawakuhitimu huku mwaka 2015 idadi ya wanafunzi ambao hawakumaliza masomo yao ikiongezeka na kufikia 160 sawa na asilimia 22.9  wakati huo kwa mwaka 2016 wanafunzi 149 sawa na asilimia 20 ya wanafunzi wote waliokuwa wamesajiliwa wakishindwa kuhitimu elimu ya sekonadri.. Aidha ametaja sababu nyingine inayosababisha wanafunzi kutohitimu elimu ya Sekondari ni pamoja na jamii ya wafugaji wanaohama hama katika wilaya ya Mlele hal...

NDUGU 6 MKOANI RUKWA WAHUKUMIWA KUNYONGWA-Septemba 27,2017

Image
Na.Issack Gerald-Sumbawanga Rukwa NDUGU sita wa familia moja wamehukumiwa kifo kwa kunyongwa baada ya kuthibitika Kuwa walimuua ndugu yao wakimtuhumu Kuwa ni mchawi.

MBUNGE JIMBO LA NSIMBO ATUHUMIWA KUJIHUSISHA NA RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA UVCCM WILAYANI MPANDA KATAVI -Septemba 27,2017

Image
Mbunge Jimbo la Nsimbo Richard Mbogo MBUNGE wa jimbo la Nsimbo wa jimbo la Nsimbo Richard Philipo Mbogo ametuhumiwa kuwa miongoni mwa watu waliohusika katika kutoa rushwa ya fedha kwa kila mjumbe aliyeshiriki katika uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya ya Vijana ya chama cha Mapinduzi CCM Wilayani Mpanda.

CHADEMA WAENDELEA NA UCHAGUZI WA VIONGOZI NGAZI YA MITAA-Septemba 27,2017

Image
Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi Chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) mkoani Katavi kimewataka wanachama wake kuwa watulivu katika kipindi cha uchaguzi mdogo unaojulikana kama chadema msingi.

CCM WILAYANI MPANDA WAPATA VIONGOZI WAKE JUMUIYA YA WAZAZI,UVCCM NA UWT-Septemba 26,2017

Image
Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi JUMUIYA ya wazazi ya chama cha Mapinduzi CCM Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,imemchagua Bw.Abdalah Mtwenya Kapongolola kuwa mwenyekiti atakayeiongoza jumuiya hiyo mpaka mwaka 2022.

TRENI YA MPANDA-TABORA YAKWAMA KWA SAA 24-Septemba 25,2017

Image
Na.Issack Gerald-Mpanda Zaidi ya abiria 200 walikwama kusafiri siku ya jana kwa treni kutoka Mkoani Katavi kwenda mikoa mingine kupitia Mkoani Tabora.

VYAMA VYA WATU WENYE ULEMAVU MKOANI KATAVI VYAOMBA UKAMATAJI WATU WENYE ULEMAVU UZINGATIE HALI ZAO WANAPOTUHUMIWA KUFANYA KOSA-Septemba 23,2017

Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi VYOMBO vya ulinzi na usalama Mkoani Katavi vimeombwa kutotumia nguvu kubwa katika kuwakamta watu wenye ulemavu na badala yake watumie wataalamu kwa kujali hali za ulemavu walizonazo.

MWANAMKE MKOANI RUKWA AMJERUHI MMEWE KWA KISU AKIDAI ANAKATIZWA STAREHE YA KUNYWA POMBE-Septemba 23,2017

Na.Issack Gerald-Naksi Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Maria Mwanahiya  mkazi wa  kijiji cha Ntatumbila  wilaya Nkasi mkoani Rukwa  amemjeruhi vibaya mume wake kwa kumchoma kisu ubavuni kwa madai kuwa alipata hasira baada ya kukerwa na kitendo cha mume wake kumlazimisha kuacha starehe zake ikiwemo kunywa pombe.

RAIS MAGUFULI ATANGAZA AJIRA 3000 ZA WANAJESHI WAPYA-Septemba 23,2017

Image
Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa nchi Dkt. John Pombe Magufuli, ametangaza kutoa ajira kwa wanajeshi 3000 wapya mwaka huu,ili jeshi la Tanzania liwe na askari wa kutosha.

MWILI WA ASKARI WA JWTZ KUAGWA JUMATATU-Septemba 23,2017

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema mwili wa marehemu Praiveti Mussa Jumanne ambaye ameuawa nchini DRC uanatarajiwa kuagwa Jumatatu ya wiki ijayo.

RAIS WA ZANZIBAR ATEUA VIONGOZI WA TAASISI MBALIMBALI-Septemba 23,2017

Image
Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi wapya na kufanya mabadiliko katika baadhi ya taasisi mbalimbali za Serikali.

TANROADs MKOANI KATAVI WATAJWA KUSABABISHA AJALI-Septemba 22,2017

Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi BAADHI ya wakazi wa wanispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameilalamikia Wakala wa barabara TANROADs Mkoani Katavi kwa kupuuzia uwekaji alama za usalama barabarani katika eneo la Super City mtaa wa Majengo eneo ambalo limekuwa likisababisha ajali mara kwa mara.

TLB KATAVI WASUBIRI MWONGOZO ILI KUSHIRIKI SIKU YA FIMBO NYEUPE DUNIANI-Septemba 22,2017

Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi CHAMA cha watu wasioona Mkoani Katavi (TLB) kimesema kinasubiri mwongozo wa viongozi wa chama hicho ngazi ya Taifa ili wafahamu namna watakavyoshiriki maadhimisho ya siku ya watu wasioona duniani yanayotarajiwa kuadhimishwa mwezi ujao.

SERIKALI KUMALIZA KERO ZOTE ZA MAJI-WAZIRI MKUU-Septemba 21,2017

Image
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na huduma ya umeme katika maeneo mbalimbali nchini zikiwemo wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.

WAKAZI KATAVI WALALAMIKIA KUKITHIRI KWA TAKA KATIKA MAKAZI YAO-Septemba 21,2017

WAKAZI wa kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda wamelalamikia uwepo wa taka katika makazi yao kwa muda mrefu hali inayosababisha kuhofia magonjwa ya mlipuko.

KIWANDA CHAKOSA CHOO,WANANCHI WAKERWA NA HARUFU MBAYA,MWENYE KIWANDA ARONGA-Septemba 21,2017

Kiwanda cha kupasulia magogo kilichopo kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi chenye zaidi ya wafanyakazi 20 hakina huduma ya choo.

ZITTO AREJEA NCHINI BAADA YA KUMJULIA HALI TUNDU LISSU,SASA AMESEM AHAYA HAPA MH.ZITTO-Septmba 18,2017

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amefunguka na kudai amerudi nchini akiwa na unyenyekevu mkubwa zaidi kwa sababu ya nguvu na ujasiri alioonyeshwa na Mbunge Tundu Lissu pindi alipokwenda kumjulia hali katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

ASKARI WAWILI WAHUKUMIWA JERA MIAKA 35-Septemba 18,2017

Image
Mahakama Kuu ya Tanzania imewahukumu askari Polisi wawili wa kutoka kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam na watu wengine sita kwenda jela miaka 35 kwa makosa mawili ya kukutwa nyara za serikali na kujihusisha na mtandao wa ujangili.

WAKAZI WILAYANI MPANDA MKOANI KATAVI WATAKIWA KURIPOTI UKATIRI WA KIJNSIA-Septemba 18,2017

WANANCHI wilayani Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kufichua matukio ya ukatiri wa kijinsia yanayofanyika na kupelekea madhara kwa wanaotendewa.

JESHI LA POLISI WILAYANI MPANDA LAWATAKA WANANCHI KURIPOTI MATUKIO KWA WAKATI ILI KUDHIBITI UHARIFU-Septemba 18,2017

JESHI la polisi Wilayani Mpanda Mkoani Katavi limewataka wananchi kushirikiana na jeshi hilo kuripoti kwa wakati matukio mbalimbali ya kiuharifu yanayoendelea kutokea wilayani Mpanda.

NDOA ZA JINSIA MOJA ZAMFIKISHA MAHAKAMANI-Septemba 16,2017

Image
Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Sharifu Issah maarufu kama Zamda Salumu Mkazi wa Manispaa ya Mtwara, amefikishwa mahakamani kwa kosa la kufanya vitendo vya utovu wa kimaadili kwa kujifanya mwanamke na kumshawishi mwanaume mwenzake kufunga ndoa.

MLIPUKO WA KIPINDUPINDU MBEYAWATU 8 WAFARIKI DUNIA 628 WAPATIKANA NA UGONJWA HUO-Septemba 16,2017

Image
DC Wilayani Mbarali Reuben Mfune Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya Mh.Reuben Mfune ameagiza bar zote,migahawa,vilabu vya pombe na grocery kufungwa kwa siku zisizojulikana kutokana na ugonjwa wa kipindupindu kuzidi kusambaa wilayani humo.

WAPENZI WA JINSIA MOJA WAKAMATWA ZANZIBAR-Septemba 16,2017

Mamlaka ya kisiwani Zanzibar imewakamata watu 20 wanaotuhumiwa kushiriki katika mapenzi ya jinsia moja.

UNDENI VIKUNDI FEDHA KWA AJILI YA WATU WENYE ULEAMAVU ZIPO-Septemba 16,2017

SIKU moja baada ya Shirikisho la watu wenye Ulemavu Shivyawata Mkoani Katavi kuomba watu wenye ulemavu kuwezeshwa ili kujikwamua kimaisha na hatimaye kujenga uchumi wa taifa,halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi imewataka watu wenye ulemavu kuunda vikundi vya kijasiliamali ili wapatiwe mikopo.

MKUU WA MKOA RUKWA AWA MBOGO KUHUSU UVUVI HARAMU-Septemba 15,2017

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zelote Stephen ameionya idara ya uvuvi mkoani humo kuacha mzaha katika suala zima la kupambana na wavuvi haramu kwani ikifanya mzaha vizazi vijavyo vitabaki vikiwashuhudia viumbe wa kwenye maji katika picha na mikanda ya video kama katika mataifa Mengine yalivyo. 

SHIVYAWATA WAOMBA WATU WENYE ULEMAVU WAWEZESHWE ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI-Septemba 15,2017

Image
SHIRIKISHO la vyama vya watu wenye ulemavu Shivyawata Mkoani Katavi,limesema watu wenye ulemavu mkoani Katavi bado wanahitaji kuwezeshwa zaidi kama makundi mengine yasiyo na ulemavu ili kujikwamua kimaisha na kujenga uchumi wa taifa.

TANZANIA YASHTUSHWA KUHUSISHWA NA KOREA KASKAZINI-Septemba 16,2017

Image
Tanzania imesema imeshtushwa baada ya kuorodheshwa miongoni mwa nchi ambazo zimechunguzwa na Umoja wa Mataifa na kuhusishwa kuwa na uhusiano wa kibiashara na Korea Kaskazini.

AJALI YA BOTI MKOANI RUKWA,YAUA WENGINE HAWAJAJULIKANA WALIPO-Septemba 14,2017

MTOTO aliyefahamika kwa jina Yakini Said umri wa mwenye miaka miwili amekufa maji na wengine kumi na moja kuokolewa Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa baada ya boti waliyokuwa wakisafiria katika ziwa Tanganyika kupinduka.

MTU MMOJA AUWAWA KATAVI AOKOTWA KANDO KANDO YA BARABARA-Septemba 14,2017

Image
ACP Damas Nyanda MTU mmoja ambaye hajafahamika jina wala makazi yake,amekutwa akiwa amekufa baada ya kuuwawa na watu wasiofahamika na kisha mwili wake kutupwa kando kando ya barabara Wilayani Mpanda Mkoani Katavi.

AKAMTWA NA SILAHA YA KIVITA AINA SMG AKIJIHUSISHA NA UHALIFU NDANI NA NJE YA MKOA WA KATAVI-Septemba 14,2017

Image
Mfano wa silaya aina ya SMG JESHI la polisi Mkoani Katavi linamshikilia mtu mmoja pamoja na silaha ya kivita aina ya SMG yenye risasi 30 aliyokuwa akiitumia katika uharifu mbalimbali.

RC RUKWA AWAOMBA MADHEHEBU YA DINI KUENDELEA KUIOMBEA NCHI IWE NA AMANI-Septemba 14,2017

Image
Mhashamu baba Askofu kanisa Katholic jimbo la Sumbawanga Damian Kyaruzi MKUU wa Mkoa wa Rukwa Zelote Stephen amewaomba waumini wa madhehebu yote yaliyopo mkoani humo kuendelea kuiombea nchi amani kwani serikali ipo imara katika kuhakikisha inasimamia misingi ya sheria.

WAWILI WAFARIKI DUNIA KWA AJALI MKOANI RUKWA-Septemba 14,2017

WATU wawili Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa,wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kuanguka.

AUWAWA KWA NGUMI NA MATEKE AKITUHUMIWA KUTOHUDHURIA MSIBA WA KAKA YAKE-Septemba 14,2017

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Frank Mwanarusi(32) mkazi wa katika kijiji cha Ilemba Mjini Laela Mkoani Rukwa,ameuawa na watu sita baada ya kupigwa mateke na ngumi sehemu za ubavu wa kulia na kushoto.

TANESCO MKOANI KATAVI WAMEWASHA UMEME WA REA WILAYANI MLELE-Septemba 13,2017

Image
SHIRIKA la umeme Nchini Tanesco Mkoani Katavi limewasha umeme wa mradi wa umeme vijijini Rea Wilayani Mlele Mkoani Katavi na kuwataka wananchi Wilayani humo hususani wakazi wa mji wa Inyonga ambayo ni makao Makuu ya Wilaya watandaze nyaya zao katika nyumba ili waunganishiwe umeme.

WAKAZI KATAVI WALALAMIKIA MATUSI YA WAGUZI NA KUNYIMWA MATIBABU-Septemba 12,2017

Baadhi ya wakazi wa Kata ya Katumba Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi,wamewalalamikia baadhi ya wauguzi na madaktari wa kituo cha afya cha Katumba na Zahanati ya Kaminula kutokana na  lugha ya matusi kwa wagonjwa inayoambatana na kutopatiwa matibabu ipasavyo.

KATIBU MKUU CHADEMA AGOMA KUJISALIMISHA POLISI ILI AOHJIWE SAKATA LA TUNDU LISSU-Septemba 11,2017

Image
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema hawezi kwenda kuripoti Polisi kama alivyotakiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto kwa kuwa hakuambiwa siku maalumu ya kwenda.

RAIS MAGUFULI AOGOPA KUPOKEA MAJINA YA WAFUNGWA WANAOTAKIWA KUNYONGWA-Septemba 11,2017

Image
Rais John Pombe Magufuli amesema kama rais anaogopa kusaini ili wanyongwe baadhi ya wafungwa ambao wamehukumiwa kunyongwa kutokana na makosa mbalimbali.

JAJI MKUU MPYA TANZANIA AAPISHWA RASMI-Septemba 11,2017

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemuapisha Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye amemteua kushika wadhifa huo Septemba 10, mwaka huu .

MJI WA NAMANYERE NKASI KUJENGEWA LAMI KABLA YA 2020-Septemba 11,2017

Image
SERIKALI imesema inatarajia kukamilisha ujezi wa barabara yenye urefu wa kilomita tano kwa kiwango cha lami Mjini Namanyere Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa kama iliyoaihidiwa na serikali wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015.

JUMUIYA YA KUHIFADHI TAMADUNI,MILA NA DESTURI ZA KITANZANIA KANDA YA ZIWA TANGANYIKA YAOMBA KUJENGEWA MAKUMBUSHO-Septemba 11,2017

Image
JUMUIYA ya kuhifadhi,kudumisha na kuendeleza mila na desturi za Tanzania katika ukanda wa ziwa Tanganyika, wameiomba serikali ya awamu ya Tano kusaidia ujenzi wa makumbusho yaliyopangwa kujengwa mkoani Katavi kama walivyoahidiwa na serikali ya awamu ya nne.

RC TABORA ATOA MWEZI MMOJA KIWANDA CHA KUZALISHA MAFUTA YA PAMBA KIWE KINAFANYA KAZI-Septemba 10,2017

Image
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imetoa mwezi mmoja kwa wamiliki wa Kiwanda cha Pamba cha Manonga kuhakikisha wamekikarabati ili kiweze kuanza tena uzalishaji wa mafuta ya pamba na uchambuzi wa Pamba na kutengeneza ajira kwa vijana mkoani hapo.

RAIS JOHN MAGUFULI ATEUA JAJI MKUU WA TANZANIA-Septemba 10,2017

Image
Rais Magufuli akiwa na Jaji mteule Jaji Prof.Ibrahim Hamis Juma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli leo amemteua Mhe.Prof.Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

WAKUU WA MIKOA 10 AKIWEMO WA KATAVI WAAGIZWA KUSIMAMIA ZAO LA KILIMO-Septemba 10,2017

Image
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa mikoa 10 inayolima pamba nchini akiwemo mkuu wa mkoa wa Katavi,kusimamia zao hilo kwa karibu ili kuinua uzalishaji wake na kuwaongezea kipato wananchi.

MBUNGE MCHUNGAJI PETER MSIGWA AELEZA KUTORIDHISHWA NA KAULI YA IGP SIRRO-Septemba 10,2017

Image
Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA) Mchugaji Peter Msigwa amefunguka na kuonyesha kutoridhishwa na kauli ya  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,IGP Simon Nyakoro Sirro kusema Tundu Lissu hakuwahi kutoa taarifa juu ya watu wanaomfuatilia.

ASKOFU GWAJIMA AFUNGUKA KUHUSU UHARIFU UNAOENDELEA HAPA NCHINI ASHANGAA VIONGOZI WA DINI KUWA KIMYA-Septwemba 10,2017

Image
Askofu Josephat Gwajima ASKOFU Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima amefunguka na kudai anawashangaa viongozi wa kiroho wanaokaa kimya na kuacha masuala ya uhalifu yakiendelea katika nchi bila ya kusema lolote juu ya hilo.

SUMATRA,KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI MKOANI RUKWA WATAKIWA KUTOA ELIMU ILI KUDHIBITI AJALI-Septemba 9,2017

Image
JESHI la polisi Mkoani Rukwa limeitaka mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumtra pamoja na kikosi cha  usalama barabarani kujitahidi kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara.

TUNDU LISSU APIGWA RISASI APELEKWA CHUMBA CHA UPASUAJI DODOMA-Septemba 7,2017

Image
Mh.Tundu Lissu Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi nyumbani kwake na kwamba hali yake ni mbaya.

WAZIRI SIMBACHAWENE AJIUDHULU KWA AGIZO LA RAIS MAGUFULI-Septemba 7,2017

Image
Mh.George Simbachawene Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,George Simbachawene ameandika barua ya kujiudhulu wadhifa huo baada ya kutajwa katika ripoti za uchunguzi wa biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi iliyoonyesha namna serikali lilivyopoteza matrilioni ya fedha kutokana na sababu mbalimbali. Waziri Simbachawene ameandika barua hiyo muda mfupi baada ya Rais Magufuli kuwataka viongozi wote aliowateua na wametajwa katika ripoti hiyo wakae pembeni ili kupisha uchunguzi ambao utakuwa huru na wa haki. Mbali na Simbachawene,wengine waliokuwa wametakiwa kukaa pembeni ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Edwin Ngonyani ambaye alituhumiwa kutotekeleza majukumu yake kikamilifu alipokuwa akifanya kazi katika Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) lenye dhamana ya kusimamia madini. Mbali na Ngonyani,mwingine ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara,Eliakim Maswi baye naye amepaswa kupisha uchunguzi ambapo Rais ameagiza ufa...