WAKAZI WILAYANI MPANDA MKOANI KATAVI WATAKIWA KURIPOTI UKATIRI WA KIJNSIA-Septemba 18,2017
WANANCHI wilayani Mpanda Mkoani
Katavi wametakiwa kufichua matukio ya ukatiri wa kijinsia yanayofanyika na
kupelekea madhara kwa wanaotendewa.
Kauli hiyo imetolewa na Mkaguzi wa
Polisi Wilayani Mpanda ambaye pia ni kaimu mkuu wa Kituo cha Polisi Insepcta
Stephen Kisaka ambapo amesema makundi ya watoto na wanawake yanaathirika kwa
kiasi kikubwa.
Kwa upande wake Afisa wa dawati na
jinsia na watoto Wilayani Mpanda ambaye pia ni Polisi Kata Kata ya Makanyagio
Inspecta Mwanaisha Lwano,wamawataka wananchi kutoa taarifa za ukatiri kwa
watoto,wanawake na makundi mengine ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.
Kwa upande wao wananchi wameahidi
kutoa ushirikiano ili kutokomeza matukio ya unyanyasaji wa kijinsia.
Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa
inayotajwa kuwa na ukatiri kwa kiwango kikubwa ambapo miongoni mwa chanzo ni
mfumo kandamizi kwa baadhi ya familia.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments