ASKARI WAWILI WAHUKUMIWA JERA MIAKA 35-Septemba 18,2017
Mahakama
Kuu ya Tanzania imewahukumu askari Polisi wawili wa kutoka kituo cha Oysterbay
jijini Dar es Salaam na watu wengine sita kwenda jela miaka 35 kwa makosa
mawili ya kukutwa nyara za serikali na kujihusisha na mtandao wa ujangili.
Hayo
yamesemwa na Wakili wa Serikali, Salimu Msemo alipokuwa akizungumza na waandishi
wa habari mjini Dodoma,ambapo aliwataja polisi hao wa zamani waliokutwa na
hatia ni wenye namba D 8656 CPL Senga Nyembo na G 553 PC Issa Mtama washtakiwa
walikutwa na meno 70 ya tembo yenye thamani ya Sh. milioni 800.
Wengine
sita waliokuwa nao wote wamekutwa na hatia ni pamoja na Prosper Maleto, Seif
Mdumuka, Amri Bakari, Said Mdumuka, Ramadhan Athuman na Musa Mohamed.
Aidha,
amesema kuwa washtakiwa hao walikutwa na kosa hilo katika eneo la kituo cha
ukaguzi cha Kauzeni lililopo Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani kabla ya
kufikishwa kortini na kukumbana na adhabu hiyo.
Hata
hivyo,ameongeza kuwa katika kosa la kwanza, washtakiwa walihukumiwa kwenda jela
miaka 20 kila mmoja na faini kwa kila mmoja, wakati katika kosa la pili,
washtakiwa wawili ambao ni hao polisi, walihukumiwa miaka 15 kwenda jela.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Ukurasa wa Facebook:P5Tanzania Limited na Issack Gerald
0764491096
Comments