JESHI LA POLISI WILAYANI MPANDA LAWATAKA WANANCHI KURIPOTI MATUKIO KWA WAKATI ILI KUDHIBITI UHARIFU-Septemba 18,2017
JESHI la polisi Wilayani Mpanda
Mkoani Katavi limewataka wananchi kushirikiana na jeshi hilo kuripoti kwa
wakati matukio mbalimbali ya kiuharifu yanayoendelea kutokea wilayani Mpanda.
Wito huo umetolewa na kaimu mkuu wa
Kituo cha Polisi Wilayani Mpanda Insepcta Stephen Kisaka ambaye pia ni Mkaguzi
wa Polisi katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika mtaa wa Mpadeco
kata ya Makanyagio.
Aidha Inspecta Kisaka ambaye pia ni
mlezi wa kata ya Makanyagio amewatoa hofu wananchi kuwa siri za kiuharifu watakazozita
zitahifadhiwa kwa kuwa jeshi la polisi kwa sasa linatunza siri ipasavyo kwa
lengo la kutokomeza uharifu.
Kwa upande wake Polisi Kata Kata ya
Makanyagio Inspecta Mwanaisha Lwano,wamawataka wananchi kutoa taarifa za
ukatiri kwa watoto,wanawake na makundi mengine ili wahusika wachukuliwe hatua
za kisheria.
Naye Mwenyekiti wa mtaa wa Mpadeco
Bw.Benard Nkana ameagiza wenye nyumba wote katika mtaa huo kutopangisha watu au
wageni katika nyumba zao bila kutoa taarifa kwa viongozi kinyume na hapo hatua
za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mwenye nyumba.
Nao baadhi ya wananchi wa mtaa wa
Mpadeco akiwemo Julius Kipeta wameomba vikundi vya ulinzi shirikishi vitakavyoundwa
viwezshwe mipkopo kwa ajili ya shghuli za maendeo huku wengine wengine wakitaka
ukaguzi wa waharifu ufanyike nyumba kwa nyumba vijana watakaobainika
kujihusisha na uharifu wawajibishwe pamoja na wazazi wao kwa kushindwa kama
sehemu ya waharifu.
Mkutano huo pia umehudhuriwa na
aliyekuwa mstahiki meya wa Manispaa a Mpanda na diwani wa kata ya Mpanda Hotel
Bw.Enock Gwambasa huku karibu watu 80 wakihudhuria mkutano huo.
Miongoni mwa uharifu ambao umekuwa
ukitokea mara kwa mara katika mtaa wa Mpadeco ni pamoja na wizi wa mali za
nyumbani kama mifugo,pamoja na simu
unaofanyika mara nyavu za madirisha zinapokuwa zimekatwa na vibaka hasa nyakati
za usiku.
Wakati huo huo ajenda nyingine
zilizojadiliwa katika mkutano huo ni ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa
katika shule ya msingi Katavi pamoja na zoezi la usafi wa mtaa ambapo kwa
upande wa vyumba vya madarasa wananchi wametakiwa kuchangia asilimia 20 ya
nguvu ya wananchi kama kuchangia maendeleo ambapo ni sawa na matofali laki 2
kwa kila mtaa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa pamoja na kuendelea kuchangia Shilingi
2,000/= kwa ajili ya kuchangia gharama za uzoaji taka.
Mtaa wa Mpadeco ni miongoni mwa mitaa
mitano ya Kata ya Makanyagio ambapo mitaa mingine ni Kigoma,Mwangaza, Kachoma
na Makanyagio ambapo jumla yanahitajika matofali milioni moja kwa ajili ya
ujenzi wa madarasa.
Comments