MTU MMOJA AUWAWA KATAVI AOKOTWA KANDO KANDO YA BARABARA-Septemba 14,2017

ACP Damas Nyanda
MTU mmoja ambaye hajafahamika jina wala makazi yake,amekutwa akiwa amekufa baada ya kuuwawa na watu wasiofahamika na kisha mwili wake kutupwa kando kando ya barabara Wilayani Mpanda Mkoani Katavi.

Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda amesema tukio hilo la mauaji limetokea usiku wa kuamkia jana maeneo ya kata ya Machimboni.
Aidha ACP Nyanda amesema baada ya kuchunguza mwili wa marehemu,umekutwa ukiwa umejeruhiwa vibaya ambapo inadhaniwa kuwa wauaji walimpiga na kitu kizito.
Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda kusubiri taratibu nyingine za mazishi ambapo wahusika bado wanatafutwa na jeshi la polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Wakati huo huo Jeshi la polisi Mkoani Katavi limetoa wito kwa wakazi mkoani Katavi kuacha kujichukulia sheria mkononi ili kuepuka mkondo wa sheria kwa kuwa suala la kuua siyo jukumu lao.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

0764491096

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA