AJALI YA BOTI MKOANI RUKWA,YAUA WENGINE HAWAJAJULIKANA WALIPO-Septemba 14,2017
MTOTO
aliyefahamika kwa jina Yakini Said umri wa mwenye miaka miwili amekufa maji na
wengine kumi na moja kuokolewa Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa baada ya boti
waliyokuwa wakisafiria katika ziwa Tanganyika kupinduka.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Rukwa George Kyando amesema ajali hiyo ambayo ilitokea jana ikihusisha
boti ambayo mpaka sasa haijajulikana jina wala mmiliki wake ilikuwa imebeba abiria
kumi na nne ikitokea iktokea kijiji cha kilando wilayani
Nkasi ikielekea Kijiji cha Kyala Mkoani
Kigoma ambapo hata hivyo watoto wawili mpaka sasa hawajaonekana na
wanahofiwa kuwa huenda nao wamepoteza maisha huku wamiliki ambao nao walikuwa
miongoni mwa abiria wakitokomea kusikojulikana.
Hivi
punde kabla ya kuingia mitamboni mwenzangu Edward Mganga amezungumza na Kamanda
wa Polisi Mkoani Rukwa George Kyando kuhusiana na ajali hiyo.
Chanzo
cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni hali ya hewa ambapo kulikuwa na upepo mkali
ziwani uliopelekea hata baadhi ya nyumba kuezuliwa mjini Namanyere Wilayani
Nkasi.
Mwili
wa marehemu umekabidhiwa kwa wazazi wake ambao nao walikuwa ni miongoni mwa abiria kwa ajili ya mazishi.
Wakati
huo huo Kamanda wa Polisi Mkoani Rukwa Kamishna Msaidizi wa Polisi George
Kyando amewataka
wananchi hasa watumiaji wa vyombo vya majini kuwa makini na kiwango cha watu na
mizigo inayobeba na kuhakikisha hawazidishi uzito ili kuzuia ajali zisizo na ulazima.
Aidha
Pia amewashauri waendesha vyombo hivyo kuzingatie sana suala la hali ya hewa kwa
kuwa ndicho chanzo kikubwa cha ajali kama hizo.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments