AKAMTWA NA SILAHA YA KIVITA AINA SMG AKIJIHUSISHA NA UHALIFU NDANI NA NJE YA MKOA WA KATAVI-Septemba 14,2017
Mfano wa silaya aina ya SMG |
Kwa mjibu wa Kamanda wa Polisi Mkoani
Katavi Kamanda wa polisi mkoani katavi Damas nyanda amesma kuwa mtu huyo ambaye
amehifahiwa jina lake kwa sababu za kiupelelezi alikamatwa maeneo ya kibaoni.
Kamanda Nyanda amesema baada ya
kumkamata mtuhumiwa alisema silaha imehifadhiwa Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa na
hatimaye mke wa mtuhumiwa kuwakabidhi jeshi la polisi silaha aina ya SMG ikiwa
na risasi hizo 30 ambapo imeelezwa kuwa silaha hiyo ndiyo iliyokuwa ikitumika
katika uharifu wa aina mbalimbali ndani na nje yua mkoa wa Katavi.
Aidha jeshi la polisi Mkoani Katavi
limesema linaendelea na oparesheni ya kuwatafuta wahusika wa uhalifu wa ain
ambalimbali mkoani Katavi ambapo mpaka sasa wamefikia vijiji 101 ambavyo
wamevifanyia oparesheni.
Kufuati tukio hilo kamanda Kamanda Nyanda
ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi katika kuibua matukio
mbalimbali yanayojitokeza ndani ya jamii ili kuyakomesha.
0764491096
Comments