WAWILI WAFARIKI DUNIA KWA AJALI MKOANI RUKWA-Septemba 14,2017
WATU
wawili Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa,wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa
wakisafiria kuacha njia na kuanguka.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Rukwa ACP George Kyando amesem ajali hiyo imetokea juzi
ikihusisha gari lenye namba za usajili T
232 BDG aina ya Howo Mixer lililokuwa likisafirisha zege katika barabara ya
Chala Namanyere.
Kamanda
amewataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Shabani Supa(31) mkazi wa
Tabora na Gaudensia Ernest(33).
Chanzo
cha ajali hiyo kimebainika kuwa ni mwendo kasi wa dereva ambapo kamanda Kyando
amesema dereva huyo ambaye hajafahamika jina lake amekimbia baada ya ajali hiyo
huku juhudi za kumtafuta zikiendelea.
Aidha
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Kamishna Msaidizi wa Polisi George Kyando ametoa
wito kwa wananchi wote hasa watumiaji wa vyombo vya moto na watumiaji wa
barabara kuwa makini na kufuata sheria
na alama za usalama barabarani ili kuzuia ajali.
Habari zaidi ni
www.p5tanzania.blogspot.com
0764491096
Comments