AUWAWA KWA NGUMI NA MATEKE AKITUHUMIWA KUTOHUDHURIA MSIBA WA KAKA YAKE-Septemba 14,2017
MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Frank Mwanarusi(32) mkazi wa katika
kijiji cha Ilemba Mjini Laela Mkoani Rukwa,ameuawa na watu sita baada ya
kupigwa mateke na ngumi sehemu za ubavu wa kulia na kushoto.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Rukwa ACP Geroge
Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nakusema tukio hilolimetokea juzi
majira ya usiku.
Kamanda
Kyando amesema chanzo cha mauaji ni ugomvi wa kifamilia wakimtuhumu marehemu
kuwa kwa kwanini hakufika kwenye msiba wa kaka yake aliyefariki Septemba 2
mwaka huu.
Kwa
mjibu wa Kamanda Kyando,wauaji walimvizia kilabuni na kumkamata na kisha kuanza
kumshambulia hadi kufa ambapo hata hivyo mtuhumiwa mmoja amekamatwa na
anatarjiwa kufikishwa mahakamani huku juhudi za kuwatafuta waliokimbia
zinaendelea.
Wakati
huo huo kamanda ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi mkoani
humo hukuwakamata watuhumiwa wa mauaji pamoja na wote wanaokuwa najichukulia
sheria mkononi.
Habari zaidi ni
www.p5tanzania.blogspot.com
0764491096
Comments