RC RUKWA AWAOMBA MADHEHEBU YA DINI KUENDELEA KUIOMBEA NCHI IWE NA AMANI-Septemba 14,2017
Mhashamu baba Askofu kanisa Katholic jimbo la Sumbawanga Damian Kyaruzi |
Ombi hilo alilitoa jana wakati akifungua mkutano wa siku nne wa
Sinodi ya kanisa la Moravian jimbo la Rukwa na Katavi,mkutano ambao umehudhuriwa
na wachungaji, makatibu,wenyeviti na wanakwaya wa mikoa yote miwili.
Alisema watanzania ni watu wanaomuamini mwenyezi mungu hivyo
basi kila mtu ahakikishe anaiombea sana nchi yetu na viongozi wake ili amani
iliyopo iendelee kudumu.
"Kama viongozi wa dini mna silaha kubwa ya kuiombea nchi
amani hivyo tunawaomba muendelee kuombea nchi amani na kuwasisitiza waumini
wafanye hivyo na niwahakikishie kuwa serikali ipo imara kuhakikisha sheria
zinafuatwa ili kuendeleza amani iliyopo."
Kwa upande wake mgeni mwalikwa Askofu wa kanisa Katoliki Jimbo
la Sumbawanga Damian Kyaluzi aliipongeza serikali kwa kuthibiti yaliyotokea
katika wilaya ya kibiti na kukemea yaliyowatokea Mh. Tundu Lisu pamoja na Meja
Generali Mstaafu Mrimbata na kuendelea kuwaombea na kuliombea taifa liendelee
kubaki na amani iliyoachwa na waasisi wa nchi hii.
Awali akisoma risala fupi ya kanisa hilo kwa mgeni rasmi
mwenyekiti wa kanisa la Moravian jimbo la Rukwa mchungaji Nobert Sikazwe
alilalamikia ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga kushindwa kuwapa
vibali vya ardhi ili waendelee kushirikiana na serikali katika kuleta
maendeleo.
Mwandishi:Gurian Adolfu
Mhariri:Issack Gerald
Habari zaidi ni
www.p5tanzania.blogspot.com
0764491096
Comments