VIBOKO MKOANI KATAVI WASABABISHA NDOA KUVUNJIKA PIA UHARIBIFU WA MAZAO SHAMBANI-Septemba 29,2017
WAKAZI wa kijiji cha Milala Kata ya
Misunkumilo katika Manispaa ya Mpanda,wameilalamikia serikali kutochukua hatua
dhidi ya viboko waliopo bwawa la Milala vinavyoharibu mazao shambani na
kutishia uhai wa binadamu mara kwa mara.
Wakazi hao wakiwemo Masoud Mawisa na
Adam Said Kanyamaso kutoka mitaa ya Kigamboni,Misunkumilo na Makanyagio
wamesema,madhara mengine ambayo yametokana na
viboko hao ni kuvunjika kwa ndoa zao kutokana na wanaume kuhamishia makazi yao
shambani ili kudhibiti
Kwa
upande wake Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Misunkumilo Bw.Antipas Kalumbete ambaye
pia ndiye anayekaimu nafasi hiyo katika kijiji cha Milala,amethibitisha viboko
hao kuwa tishio wa wakazi wa maeneo hayo akisema kuwa maliasili waliandikiwa
barua lakini mpaka sasa hakuna hatua yoyote ambayo imechukuliwa dhidi ya
wanayama hao.
Bwawa la
milala ambalo ni miongoni mwa vyanzo vya maji yanayotumika kwa wakazi wa
Manispaa ya Mpanda inasemekana kwa sasa lina viboko zaidi ya tehelathini huku
wakazi wa maeneo jirani na bwawa hilo wakilazimika kujifungia ndani majira ya
jioni wakiogopa kushambuliwa.
Viboko
hao wanadaiwa kutoka katika mto Katuma uliopo kata ya Sitalike palipo na shule
kubwa ya viboko ambapo hata hivyo hakuna uhusiano wa sitalike na bwawa la
milala kwa kuwa viboko hao wametoroka na kupitia nchi kavu ambapo umbali kutoka
Bwawa la Milala mpaka Sitalike ni takribani kilomita 60.
Kumekuwa
na matukio ya wanayama pori kutoroka katika hifadhi zao na kusababisha madhara
kwa binadamu ambapo wanyama wengine ambao wamekuwa wakitoroka katika hifadhi na
kuvamia makazi ya watu na kusababisha madhara kwa watu ni Simba.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments