WAZEE MKOANI KATAVI WAOMBA SERIKALI IWATENGENEZEE MAZINGIRA RAFIKI KATIKA MASUALA YA MATIBABU-Septemba 29,2017
Na.Issack Gerald-Katavi
UMOJA wa wazee Mkoani
Katavi kimeiomba serikali kuendelea kutengeneza mazingira yatakayomwezesha mzee
kupatiwa huduma za matibabu bila usumbufu.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa
chama hicho Mkoani Katavi Bw.Marius Bagaya wakati akizungumza na Mpanda Radio
kuhusu kuelekea maadhimisho ya siku ya wazee duniani yatakayoadhimishwa
keshokutwa.
Aidha Bagaya
amesema kutokana na Ofisi nyingi kuwa na wafanyakazi vijana,baadhi ya vijana
wanashindwa kuwahudumia ipasavyo hasa katika ofisi za umma ambapo amewaomba
vijana waliopo kaatika Ofisi mbalimbali kutambua kuwa kila mtu ni mzee
mtarajiwa.
Kwa
upande wake Makamu katibu wa Chama cha wazee Mkoani Katavi Bw.Nganyaga
Mwendambali amesema pamoja na changamoto zinazowakabili wazee,serikali imepiga
hatua katika masuala ya wazee ikiwa ni pamoja na wazee kuingizwa katika Wizara
ya afya ambapo pia ameomba wazee wapate pensheni pamoja na kutengenezewa sheria
itakayosimamia mahitaji yao.
Hata
hivyo kwa upande wa baadhi ya wazee pamojana mambo mengine wanasema kwa sasa
katika baadhi ya maeneo mkoani Katavi hawapangi msitari ambapo sera ya Mzee
kwanza inazingatiwa wanapohitaji kupatiwa huduma.
Siku ya
Jana mganga mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt.Yahya Hussein aliziagiza Halmashauri
zote Mkoani Katavi kuhakikisha zinaandaa viatmbulisho kwa ajili ya wazee ili
wapatiwe matibabu bila usumbufu ikiwa ni pamoja na huduma nyingine muhimu kwa
wazee.
Mkoa wa
katavi kwa mjibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 ulikadiriwa kuwa na
wazee wapatao 500.
Maadhimisho
ya siku ya wazee Duniani kwa mwaka 2017 yanatarajiwa kuadhimishwa mkoani Dodoma
na kauli mbiyu inasema ‘’Kuelekea uchumi wa viwanda tuthamini
michango,uzoefu na ushiriki wa wazee kwa maendeleo ya taifa’’.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments