WAKAZI KATAVI WALALAMIKIA MATUSI YA WAGUZI NA KUNYIMWA MATIBABU-Septemba 12,2017
Baadhi
ya wakazi wa Kata ya Katumba Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi,wamewalalamikia
baadhi ya wauguzi na madaktari wa kituo cha afya cha Katumba na Zahanati ya
Kaminula kutokana na lugha ya matusi kwa
wagonjwa inayoambatana na kutopatiwa matibabu ipasavyo.
Wakazi
hao ambao hawakutaka kutaja majina yao wakihofia usalama na kunyimwa matibabu
katika vituo hivyo wamesema tatizo la baadhi ya wagonjwa kunyanyaswa lipo kwa
muda mrefu ambapo limekuwa halichukuliwi hatua ya utatuzi licha ya Diwani,Afisa
Mtedaji wa Kata,Mbunge na Halmshauri kuwa na taarifa ya hali ilivyo.
Aidha
baadhi ya wakazi wa Katumba wamelalamika kufukuzwa na kunyimbwa matibabu
wanapohoji tatizo la kutokuwepo kwa umeme katika katika kituo cah afya Katumba
licha ya Shirika la wakimbizi duniani UNHCR na Kanisa la FPCT kuleta sola na
betri katika kituo hicho ambapo kwa sasa wagonjwa hao wanalazimika kwenda
wakiwa na tochi au taa kwa ajili ya mwanga.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa kituo cha afya cha Katumba Dkt.Gabriel Ngonyani
amekataa kuzungumza na Mpanda Mpanda Radio kuhusiana na malalamiko hayo kwa
madai kuwa mpaka apate kibali cha mwajiri wake.
Wakati
huo baadhi ya wagonjwa wanaotegemea kupata huduma ya afya katika zahanati ya
Kaminula akiwemo mkazi mmoja ambaye amejitambulisha kwa majina ya Vastina
Evarist wamedai wanalazimika kutopatiwa
huduma na waguguzi katika zahanati ya Kaminula mpaka wanapokuwa wamekubali
kuchota maji kwa ajili ya wauguzi na asipokubali kuchota maji inabidi arudi
nyumbani bila kupata matibabu.
Diwani
wa Kata ya Katumba Mh.Seneta Baraka amekili kupokea kwa tuhuma hizo kwa wauguzi
katika kituo cha afya cha Katumba pamoja na zahanati ya Kaminula.
Aidha
Mh.Seneta Baraka pamoja mambo mengine amesema tatizo la umeme kituo cha afya
katumba licha ya kuwa sola na betri zilinununuliwa kama wananchi wanavyodai
isipokuwa anachofahamu ni kuwa betri zilisharibika isipokuwa hana taarifa za
uhakika kuwa betri hizo zinatumiwa na watumishi wa afya wa kituo hicho katika
majumba yao ambapo amesema tayari Shilingi milioni 1 imetengwa ili kununua
betri kuondoa tatizo la ukosefu wa umeme kwa takibani mwaka mzima.
Kwa mjibu wa wakazi wa Kata ya Katumba Jumla ya Sola 11 na Betri tatu zililetwa na UNHCR pamoja na Kanisa la FPCT.
Kwa mjibu wa wakazi wa Kata ya Katumba Jumla ya Sola 11 na Betri tatu zililetwa na UNHCR pamoja na Kanisa la FPCT.
Katika
hatua nyingine kata ya Katumba yenye vijiji 16 ikiwa na wakazi zaidi ya 54,700
wanaotegemea kupata huduma za afya katika kituo cha afya Katumba wakazi hao wameongeza
kuwa licha ya Diwani,Afisa Mtedaji wa Kata,Mbunge na Halmshauri hadi ngazi ya
kuwa na taarifa ya hali ilivyo katika huduma za afya pia wamesema hali imekuwa
mbaya zaidi hasa katika huduma ya maji na miundombinu ya barabara.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
0764491096
Comments