RAIS WA ZANZIBAR ATEUA VIONGOZI WA TAASISI MBALIMBALI-Septemba 23,2017
Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali
Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi wapya na kufanya mabadiliko katika
baadhi ya taasisi mbalimbali za Serikali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jioni na Katibu
Mkuu Kiongozi, Zanzibar Dk Abdulhamid Yahya Mzee imesema Dk Idris Muslim Hija
ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,Joseph Abdalla
Meza ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na
Uvuvi.
Wengine walioteuliwa ni Juma Ali Juma amekuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko, Bakari Haji Bakari amekuwa Katibu
Mtendaji wa Baraza la Biashara la Zanzibar na Ali Khamis Juma ameteuliwa
kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko.
Iddi Haji Makame ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara
ya Fedha na Mipango, Kapteni Khatib Khamisi Mwidini ameteuliwa kuwa Mkuu wa
Wilaya ya Magharibi A, Unguja na Abeid Juma Ali ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya
ya Wete, Pemba.
Rashid Hadid Rashid ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Chakechake, Pemba na Salma Mbarouk Khatib ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Micheweni,Pemba.
Uteuzi huo umeanza Septemba 22,hivyo viongozi hao
wanatakiwa kuripoti Ikulu Septemba 24 mwaka huu saa 2:30 asubuhi kwa ajili ya
kuapishwa.
Habari
nyingine zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au kupitia P5Tanzania Limited
Comments