VYAMA VYA WATU WENYE ULEMAVU MKOANI KATAVI VYAOMBA UKAMATAJI WATU WENYE ULEMAVU UZINGATIE HALI ZAO WANAPOTUHUMIWA KUFANYA KOSA-Septemba 23,2017
Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
VYOMBO vya ulinzi na usalama Mkoani
Katavi vimeombwa kutotumia nguvu kubwa katika kuwakamta watu wenye ulemavu na
badala yake watumie wataalamu kwa kujali hali za ulemavu walizonazo.
Kauli hiyo imetolewa na
mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya watu wenye Ulemavu Mkoani Katavi SHIVYAWATA
Bw.Issack Mlela wakati akizungumzia kuhusu ukatiri hasa kwa watoto unaoendelea
katika maeneo mbalimbali mkoani Katavi.
Amesema hivi karibuni yupo mtoto
mmoja na mwenye ulemavu wa kutosikia(Kiziwi) aliteswa na vyombo vya usalama kwa
madai kuwa alikamatwa na nyara za serikali ambapo kwa mjibu wa baadhi ya raia
walidai kuwa yupo mwanaume aliyemkabidhi nyara hiyo ambayo ilikuwa nyama pori
na kasha kutoweka na hatimaye mtoto huyo akikamatwa na kuendelea kuteswa
wakijua kuwa amekataa kuzungumza kwa sababu ya kiburi bila kujua kuwa ni
kiziwi.
Kesi ya mtoto huyo imeondolewa
mahakamani baada ya asasi za kirai ikiwemo vyama vya watu wenye ulemavu Mkoani
Katavi na Ofisi za maendeleo ya jamii kuvalia njuga suala la kukamatwa kwa
mtoto huyo aliyekuwa anakadriwa kuwa na miaka 10 wakisema kuwa hana hatia
ambapo serikali mahakama iliriridhia hana kosa na mahakama kumwachiwa huru.
Kwa upande wake Kaimu Mratibu wa
mradi wa elimu Jumuishi Mkoani Katavi Bw.Stephano Masuluali ametoa wito kwa
jamii kuwafichua watoto waliofichwa majumbani ili wapatiwe haki zao kama elimu
na mahitaji mengine muhimu kwa kuwa kuendlea kuwaficha majumbani ni kuwafanyia
ukatiri.
Kesi kadhaa za watoto kufichwa
majumbani na kutopatiwa mahitaji muhimu kama elimu na chakula kama
inavyostahili zimekuwa zikiripotiwa katika asasi za kiraia na katika vituo vya
polisi mkoani Katavi.
Habari nyingine zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au P5Tanzania Limited
Comments