MWILI WA ASKARI WA JWTZ KUAGWA JUMATATU-Septemba 23,2017
JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema mwili wa
marehemu Praiveti Mussa Jumanne ambaye ameuawa nchini DRC uanatarajiwa kuagwa
Jumatatu ya wiki ijayo.
Marehemu Praiveti Mussa Jumanne aliuawa akiwa katika jukumu la
Ulinzi wa Amani na ataagwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo kuanzia saa
mbili asubuhi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa Dkt. Florens M.Turuka anatarajiwa kuongoza katika kuuaga mwili
wa Marehemu.
Habari nyingine zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au
kupitia P5Tanzania Limited
0764491096
Comments