RAIS MAGUFULI ATANGAZA AJIRA 3000 ZA WANAJESHI WAPYA-Septemba 23,2017
Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli |
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa nchi Dkt. John Pombe Magufuli,
ametangaza kutoa ajira kwa wanajeshi 3000 wapya mwaka huu,ili jeshi la Tanzania
liwe na askari wa kutosha.
Rais Magufuli ametoa taarifa hiyo leo alipokuwa akihutubia umma
mara baada ya kuwapa kamisheni maafisa wa Jeshi,katika uwanja wa Sheikh Amri
Abeid mkoani Arusha.
Aidha Rais Magufuli katika ajira hizo kutosahaulika vijana waliohitimu mafunzo ya JKT.
Rais Magufuli leo
ametoa kamisheni kwa Maafisa wa Jeshi 422 ambao wamehitimu mafunzo katika chuo
cha Monduli,hafla ambayo imekuwa ya kwanza kufanyika katika uwanja wa umma.
Habari nyingine zaidi
ni www.p5tanzania.blogspot.com
au kupitia P5Tanzania Limited
Comments