MANISPAA YA MPANDA YASHINDWA KUPELEKA WAZEE DODOMA-Septemba 30,2017
Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
UMOJA wa wazee Mkoani
Katavi umesema Manispaa ya Mpanda imeshindwa kuwezesha wazee ili kwenda
kushiriki maadhimisho ya siku ya wazee duniani yanayofanyika kila ifikapo
tarehe moja ya mwezi wa kumi.
Kwa mjibu wa makamu
katibu wa umoja wa wazee Mkoani Katavi Bw.Nganyaga Mwendambali amesema,wakati
huo huo,jioni ya leo wazee Mkoani Katavi wanatarajia kukutana kwa ajili ya
kuzungumzia maadhimisho haya na kutoa sauti ya pamoja kuhusu maadhimisho hayo.
Awali kulikuwa na taarifa
kuwa barua zinazota mwongozo kwa wakurugenzi kuwawezesha wazee washiriki
maadhimisho zilichelewa kwa wakati ambapo hata hivyo haujajulikana ikiwa
halmashauri zote tano za Mkoa wa wa Katavi zimeshindwa kupeleka wazee katika
maadhimisho.
Kwa mjibu wa sensa ya
watu na makazi ya mwaka 2012 mkoa wa Katavi ulikuwa na wazee zaidi ya elfu
tano.
Maadhimisho ya siku ya wazee Duniani,kitaifa
kwa mwaka 2017 yanatarajiwa kuadhimishwa mkoani Dodoma na kauli mbiyu inasema
‘’Kuelekea uchumi wa viwanda tuthamini michango,uzoefu na ushiriki wa wazee kwa
maendeleo ya taifa’’.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au
ukurasa P5Tanzania Limited
Comments