RAIS WA ZANZIBAR AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI WA TAASISI-Septemba 30,2017
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein,amefanya uteuzi wa viongozi katika
Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais Shein amewateua Khamis Ramadhan
Abdalla na Bibi Aziza Iddi Suweid kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar huku akimteua
Kubingwa Mashaka Simba kuwa Katibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Wengine ambao wameteuliwa ni George
Joseph Kazi ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya
Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora anaeshughulikia masuala ya
Katiba na Sheria pamoja na Kapteni Juma Haji Juma ambaye ameteuliwa kuwa Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari.
Katika uteuzi wote huo ulioanza jana
viongozi wa lioteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu, Katibu waTume ya Maadili ya
Viongozi na Naibu Makatibu Wakuu wa natakiwa kuripoti Ikulu siku ya Jumatatu tayari
kwa kuapishwa
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au
ukurasa P5Tanzania Limited
Comments