WAKAZI KATA YA MPANDA HOTEL WAELEZEA KUFURAHISHWA NA HATUA YA KUTATUA TATIZO LA MAJI-Septemba 29,2017
Na.Issack Gerald-Katavi
BAADHI ya wakazi wa kata ya Mpanda
Hotel Manispaa ya Mpanda wameelezea kufurahishwa na hatua ya uchimbaji mitaro
ya kupitisha mabomba kwa ajili ya kuleta huduma ya maji katika katika kata
hiyo.
Wakazi hao wakiwemo Anna Fabian
Katikisha na Omerina Vyakuziwa,wamesema ikiwa maji ya kutosha yataletwa
kutaondoa tatizo la maji ambalo limekuwepo kwa zaidi ya miaka thelathini.
Aidha wakazi hao wamesema kwa muda
mrefu wamekuwa wakitegemea maji kutoka kata jirani za Makanyagio, Misunkumilo, Mwangaza
na Magereza.
Katika hatua nyingine wamesema kutokana
na uhaba kwa maji muda mrefu katika kata hiyo,hata matumizi ya vyoo vya kisasa imekuwa
changamoto kuvitumia kwa kuwa vinategemea maji.
Julai 22
mwaka huu,diwani wa kata ya Mpanda Hotel Willium Liwali alisema kata ya Mpanda
Hotel imepata zaidi ya Shilingi milioni 21 ili kukabiliana na tatizo la maji
ambalo limeikumba kata hiyo kwa muda mrefu.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments