HALMASHAURI ZOTE MKOANI KATAVI ZATAKIWA KUANDAA VITAMBULISHO VYA WAZEE-Septemba 28,2017
Na.Issack
Gerald-Katavi
Halmashauri zote Mkoani Katavi zimetakiwa kuandaa
vitambulisho kwa wazee wote waliokidhi vigezo vya kupatiwa matibabu bure.
Kauli hiyo imetolewa na Mganga Mkuu
wa mkoa wa katavi Dk. Yahaya Hussen wakati akizungumza na Mpanda Redio na
kusema kuwa hatua hiyo itarahisisha utambulisho kwa wazee ambao hawana kadi za
matibabu.
Dk Yahaya ametaja vigezo ambavyo mzee
anapaswa kupatiwa matibabu bure kuwa ni kuanzia umri wa miaka 60 pamoja na
uwezo wa maisha.
Kuhusu suala la mzee kupewa
kipaumbele katika matibabu Dk. Yahaya amesema katika wilaya ya Mpanda ipo
zahati kwa ajili ya matibabu kwa wazee sambamba na kuweka matangazo ya Mpishe
mzee apate matibabu katika zahanati na
vituo vyote vya Afya.
Kwa mjibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012,mkoa wa Katavi ulikuwa na wazee zaidi ya elfu tano(5000).
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments