SUMATRA,KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI MKOANI RUKWA WATAKIWA KUTOA ELIMU ILI KUDHIBITI AJALI-Septemba 9,2017
JESHI la polisi Mkoani Rukwa limeitaka
mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumtra pamoja
na kikosi cha usalama barabarani kujitahidi
kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara.
Kauli
hiyo imetolewa na Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani humo ACP George Kyando
wakati akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake.
Kamanda
Kyando amesema Sumtra pamoja
na kikosi cha usalama barabarani kujitahidi
kutoa elimu hasa watumia vyombo vya moto kuwa makini wanapokuwa barabarani kwa
kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani huku wakiwajali watembea kwa
miguu.
Kauli
ya jeshi hilo inakuja baada ya juzi watu wawili kufariki kwa ajali na wengine
sita kujeruhiwa katika matukio mawili tofauti ambapo chanzo kikuu kimebainika
kuwa ni mwendokasi wa madereva wa vyombo vya ufasiri.
Kamanda wa Polisi Mkoani Rukwa ACP
George Kyando juzi Septemba 7 katika kijiji cha Kamawe kata ya Sundu ambapo kulitokea
ajali ambayo ilihusisha gari aina ya Noah yenye namba za usajili T
549 DFK Noah mali ya kanisa la Moravian Mwimbi ikiendeshwa na dereva mwenye
umri wa miaka 40 na ilisababisha vifo vya watu wawili ambao ni Winfrida Simoni(35) na mtoto
Shama Charula(mwaka mmoja) wote wakazi wa kijiji cha Mwimbi.
Aidha kamanda Kyando amewataja
waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Joyce Namzyemba(27),Dalila Kalito,Rucia
Pesa(30),Jeneroza Nkasu na Balubina Ndasi wote wakazi wa kijiji cha Mwimbi.
Aidha ajali nyingine iliyotokea juzi kijiji
cha Tamasenga Manispaa ya Sumbawanga ikihusisha gari yenye namba za usajili STK
360 Mali ya Halimashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ikiendeshwa na dereva mwenye
umri wa 48 ilimgonga mtembea kwa miguu mtoto wa miaka saba na kumsababishia
majeruhi mwilini.
Kamanda
Kyando alisema Chanzo cha ajali ni uzembe
wa dereva kutokujali watumiaji wengine wa barabara.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments