TRENI YA MPANDA-TABORA YAKWAMA KWA SAA 24-Septemba 25,2017



Na.Issack Gerald-Mpanda
Zaidi ya abiria 200 walikwama kusafiri siku ya jana kwa treni kutoka Mkoani Katavi kwenda mikoa mingine kupitia Mkoani Tabora.
Baadhi ya abiria ambao walikuwa wakitegemea usafiri huo wamelalamika ubovu wa kichwa cha treni pamoja na kutopewa taarifa rasmi mara treni inapoharibika huku wakiathirika na njaa.
Kwa mjibu wa abiria ambao wamewasili Mpanda kwa treni wakitokea Tabora mpaka Mpanda wamesema,treni iliharibika mara mbili tangu Jumamosi Usiku katika wilaya ya Urambo na Kaliuwa huku wengine wakipoteza mali zao.
Hata hivyo msemaji wa kituo cha Treni Mpanda amekataa kutoa ushirikiano ili kueleza tatizo na chanzo cha treni kuangusha mabehewa mara kwa mara pamoja na kichwa cha treni kuharibika mara baada ya Mpanda Radio kufika katika Ofisi ya msemaji huyo.
Julai 24 mwaka huu,Treni hiyo inayofanya safari kutoka Mpanda mpaka Tabora ilidondosha behewa la mizigo na abiria kukwama njiani huku abiria wakipata taharuki kuhusu usalama wa maisha yao wakiwa safarini.
Wakati huo huo treni hiyo ambayo imeondoka leo kutoka Mpanda kwenda Tabora bada la jana majira ya alasiri saa tisa,abiria wake wameondoka wakiwa na wasiwasi ikiwa watafika salama kutokana na tatizo linalojitokeza mara kwa mara.
Habari nyingine zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA