MBUNGE MCHUNGAJI PETER MSIGWA AELEZA KUTORIDHISHWA NA KAULI YA IGP SIRRO-Septemba 10,2017
Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA) Mchugaji Peter Msigwa
amefunguka na kuonyesha kutoridhishwa na kauli ya Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini,IGP Simon Nyakoro Sirro kusema Tundu Lissu hakuwahi kutoa taarifa juu ya
watu wanaomfuatilia.
Mbunge Msingwa ambaye sasa yupo nchini Kenya kwenye matibabu ya
Tundu Lissu ameonyesha kusikitiswa na taarifa hiyo ya IGP.
"Kamanda Sirro Ulitaka Lissu atoe taarifa gani zaidi? Sisi
wengine ni wanasiasa, hatuna mafunzo ya kijeshi, Polisi wala Kikachero. Silaha
yetu kubwa ni kipaza sauti (microphone), kazi yetu ni kupaza sauti , hoja
inapaswa kujibiwa kwa hoja! Siyo kwa mabomu ya machozi, sio kwa virungu na
bunduki. Inaonyesha jeshi letu la polisi uwezo wake mkubwa ni kupambana na
vyama vya siasa hasa CHADEMA na CUF kuwalinda wakuu wa wilaya na mikoa"
aliandika Mchungaji Msigwa
Aidha Msigwa anasema anaumia kuona Tundu Lissu akiteseka kwa
ajili ya kutetea haki na Demokrasia ya taifa la Tanzania na kusema
alichofanyiwa Tundu Lissu kinampa ujasiri wa kusonga mbele.
"Mungu anakataza kumwaga damu isiyo na hatia! machozi
yanitoka kuona rafiki yangu Tundu Lissu akiteseka kwa kutetea haki na
demokrasia ya taifa letu, amewakosea nini? Inanipa ujasiri wa kusonga mbele,
sitanyamaza, tunakupenda Lissu wewe ndiye shujaa wetu" aliandika
Msigwa
Septemba 8, mwaka huu katika mkutano wa waandishi wa habari na kamanda
Sirro alisema Tundu Lissu hakuwahi kutoa taarifa yoyote kwa polisi juu ya gari
ambalo lilikuwa likimfuatilia kabla ya kupatwa na shambulizi hilo la kupigwa
risasi.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments