RC TABORA ATOA MWEZI MMOJA KIWANDA CHA KUZALISHA MAFUTA YA PAMBA KIWE KINAFANYA KAZI-Septemba 10,2017
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imetoa mwezi mmoja kwa
wamiliki wa Kiwanda cha Pamba cha Manonga kuhakikisha wamekikarabati ili kiweze
kuanza tena uzalishaji wa mafuta ya pamba na uchambuzi wa Pamba na kutengeneza
ajira kwa vijana mkoani hapo.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Aggrey Mwanri jana wilayani Igunga wakati alipokwenda kujionea hali halisi ya
kiwanda hicho ambacho kwa maika zaidi ya 20 hakifanyi kazi.
Alisema kuwa baada mwezi mmoja huo kukamilika
atafanya ziara Kiwandani hapo ili kuhakikisha kama ukarabati umeshakamilika na
mitambo imeshaanza kufanya kazi na kinyume cha hapo atalazimika kumwandikia
Waziri wenye dhamana na viwanda ili wamiliki wake wanyang’anye kwa ajili ya
kumpa mwekezaji mwingine.
Mwanri aliwaagiza Wamiliki wa Kiwanda hicho ambao
ni Rajani pamoja na Chama Kikuu cha Ushirika cha Igembensabo kupanga ratiba ya
mpango kazi wa utekelezaji shughuli zitakazoonyesha mipango ya ufufuaji na muda
wa ukamilishaji kwa ajili kufanikisha zoezi hilo ndani ya muda ulipangwa ,
vinginevyo watashindwa.
Mmoja wa Wabia katika Umikili wa Kiwanda cha Pamba
cha Manonga Urveshi Rajani alisema kuwa watahakikisha kuwa ndani ya mwezi mmoja
Kiwanda hicho kinakuwa tayari kwa ajili ya uzalishaji wa mafuta ya pamba na
uchambaji wa zao hilo.
Alitoa wito kwa viongozi kuhakikisha wanahamasisha
wakulima kulima pamba kwa wingi ili Kiwanda cha kiwe na malighafi za kosha kwa
ajili ya uzalishaji wa mafuta na uchambuzi wa zao hilo.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha
Ushirika cha Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) Jospeh Mihangwa alisema kuwa mitambo
ya Kiwanda cha Pamba cha Mananga ni mizuri na inasaidia kuchamba pamba bila
kukatakata na hivyo kuwa na soko kubwa duniani.
Alisema kuwa kwa sababu ya ubora wa kiwanda hicho
wao kama majirani na Mkoa wa Tabora wako tayari kushirikiana na wamiliki wake
kama watahitaji msaada wa mafundi wa kusaidia kukarabati mitambo ili kianze
tena uzalishaji kwa sababu kiwanda hicho ni muhimu sana katika uchambuzi wa
pamba.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
ya Igunga Revocatus Kuuli aliwahakikishia Wamiliki wa Kiwanda cha Pamba cha
Manongo wasiwe na wasiwasi kuhusu upatikanaji malighafi ya kutosha kwa ajili ya
kiwanda hicho,kwani uongozi umeshajipanga kuhakikisha msimu ujao wananchi
walima Pamba kwa wingi na wanavuna pamba nyingi kuliko ya msimu uliopita.
Alisema pamoja na jitihada kuwa za muda mfupi msimu
uliopita Wakulima katika Wilaya ya Igunga walifanikiwa kuzalisha kilo 10,
700,000 ,msimu ujao wanatarajia mavuno kuwa mara mbili ya kilo hizo na hivyo
kuwa malighafi nyingi kwa ajili ya viwanda..
Kiwanda hicho kinamilikiwa na Chama Kikuu cha
Ushirika cha Igembensabo kwa asilimia 20 na M/S Rajani Metals and Machinery Ltd
mwenyewe anamikili asilimia 80.
Kiwanda cha Manonga ambacho kilijengwa mwaka 1958
na Kampuni ya wafanyabiashara binafsi na mnamo mwaka 1962 Serikali
ilikitaifisha na kuipatia Kampuni ya Wakulima wa Kahama na Nzega (KANZECO) kina
miaka zaidi ya ishirini bila kufanya kazi.
Habari
zaini ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments