ASKOFU GWAJIMA AFUNGUKA KUHUSU UHARIFU UNAOENDELEA HAPA NCHINI ASHANGAA VIONGOZI WA DINI KUWA KIMYA-Septwemba 10,2017
Askofu Josephat Gwajima |
ASKOFU Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima amefunguka
na kudai anawashangaa viongozi wa kiroho wanaokaa kimya na kuacha masuala ya
uhalifu yakiendelea katika nchi bila ya kusema lolote juu ya hilo.
Mchungaji Gwajima amesema hayo akiwa Kanisa kwake leo Jumapili
ambapo aliahidi kumfanyia ibada maalum ya kumuombea mbunge wa Singida Mashariki
(CHADEMA), Tundu Lissu baada ya kupigwa risasi na watu wasiofahamika akiwa
nyumbani kwake Dodoma siku za hivi karibuni.
"Naona huruma
sana kwa watu wanaofanya uhalifu katika nchi kwa sababu unapomwaga damu ya mtu
na wewe yako itamwaga na mwingine bila ya kujarisha umemwaga kwa sababu zipi.Damu
imekuwa ikimwagika sana katika nchi hii kuanzia kule Kibiti.Nashangaa sijui
imekuwaje viongozi wa kiroho walikuwa kimya,mimi sikuwepo. Viongozi wa kiroho
ni lazima waseme",amesema Gwajima.
Aidha,Mchungaji Gwajima katika maombi yake amewataka watu
wanaofanya vitendo vya uhalifu nchini wafanye hima kutubu dhambi zao juu ya
wanachokifanya na endapo hawatafanya hivyo basi watambue yatawafika yale yale
ambayo walikuwa wakiwatendea wenzao.
"Mambo ya kiuhalifu tunatakiwa kuyakemea bila ya kuwa na
uoga wa aina yeyote wala kuangalia upande wowote ule na hivyo ndivyo Mungu
anavyotaka,unasema unachotakiwa kusema kama hiki hakipo sawa.Tundu Lissu ana
baba,mama,watoto pamoja na mke anatakiwa kuishi", amesisitiza Gwajima.
Kwa upande mwingine,Gwajima amesema hakuna jambo baya kama
kuwepo katika nchi halafu hutambui inaeleka wapi.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments