RAIS MAGUFULI AOGOPA KUPOKEA MAJINA YA WAFUNGWA WANAOTAKIWA KUNYONGWA-Septemba 11,2017
Rais John Pombe Magufuli amesema kama rais anaogopa kusaini ili
wanyongwe baadhi ya wafungwa ambao wamehukumiwa kunyongwa kutokana na makosa
mbalimbali.
Rais Magufuli amesema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaama
wakati akimuapisha Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma na kusema
anatambua kuwa idadi wa wafungwa waliohukumiwa kunyongwa ni wengi sasa ila
anaomba asipewe hiyo orodha.
"Sisi wanasiasa
tunaogopa kunyonga, natambua kuwa sasa orodha ya watu ambao wanatakiwa
kunyongwa ni kubwa sana ila mimi naomba hiyo orodha msiniletee kwa sababu najua
ugumu wake ulivyo" alisisitiza Rais Magufuli
Mbali na hilo Rais Magufuli amesema kuwa amechukua muda mrefu
kumteua Jaji Mkuu wa Tanzania kutokana na ukweli kwamba alikuwa anatafuta mtu
ambaye anaweza kuendana na dhamira yake ya kupambana na rushwa hivyo
alipojilidhisha na jaji huyo ndiyo maana ameamua kumteua kuwa Jaji Mkuu wa
Tanzania.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments