KATIBU MKUU CHADEMA AGOMA KUJISALIMISHA POLISI ILI AOHJIWE SAKATA LA TUNDU LISSU-Septemba 11,2017
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema hawezi
kwenda kuripoti Polisi kama alivyotakiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,
Gilles Muroto kwa kuwa hakuambiwa siku maalumu ya kwenda.
Kamanda Muroto amemtaka Dk Mashinji afike ofisi ya Upelelezi wa
Makosa ya jinai mkoani Dodoma au ofisi kama hiyo iliyopo Kituo cha Kikuu cha
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ili kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo
kuhusu tukio la kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu
Lissu.
“Nina taarifa za kuitwa Polisi, lakini haziko ‘specific’.
Ni wakati wowote naweza kwenda? na hawajasema nikaripoti wapi. Kwa hiyo,
wakinihitaji watakuja kuniambia,” amesema Dk Mashinji
Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 mchana
alipokuwa akielekea nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.
Kwa sasa Lissu anaendelea na matibabu katika Hospitali ya
Aga Khan jijini Nairobi, Kenya.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments