JUMUIYA YA KUHIFADHI TAMADUNI,MILA NA DESTURI ZA KITANZANIA KANDA YA ZIWA TANGANYIKA YAOMBA KUJENGEWA MAKUMBUSHO-Septemba 11,2017
JUMUIYA ya kuhifadhi,kudumisha na
kuendeleza mila na desturi za Tanzania katika ukanda wa ziwa Tanganyika,
wameiomba serikali ya awamu ya Tano kusaidia ujenzi wa makumbusho yaliyopangwa
kujengwa mkoani Katavi kama walivyoahidiwa na serikali ya awamu ya nne.
Kwa mjibu wa mwenyekiti wa jumuiya
hiyo inayojumuisha mikoa ya Rukwa,Katavi na Kigoma Bw.Michael Edward Lusambo
ambaye makazi yake yapo hapa Mkoani Katavi,amesema serikali ya awamu ya nne
iliwapatia ekari zipatazo 50 katika kijiji cha Ifukutwa Wilayani Tanganyika kwa
ajili ya ujenzi wa makumbusho hayo.
Bw.Lusambo amesema ikiwa makumbusho
hayo yatajengwa Mkoani Katavi,yatakuwa ya pili hapa nchini baada ya yaliyopo
Dar es salaam ambapo miongoni mwa malengo ni pamoja na kuwa na zahanati ya
kisasa katika makumbusho hayo.
Kwa upande wake Victory Petro
Infinula ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Mtemi Beda aliyefariki dunia mwaka
uliopita amesema serikali isaidie ujenzi huo kama inavyofanyia kazi mambo
mengine yaliyokuwa yamepangwa na serikali zilizotangulia madarakani.
Mkapa sasa kuna waganga kadhaa walio
chini ya jumuia hiyo ambapo miongoni mwa ambao wamezungumza na Mpanda Radio Fm
katika maeneo yao ya kazi wameeleza kilio chao wakiiomba serikali kuona umuhimu
wa suala hilo kama inavyotekeleza mambo mambo mengine yaliyoanzia tangu tawala
za serikali zilizopita.
Katika hatua nyingine jumuiya hii ambayo
tayari ina usajili wa kutoka serikalini imekuwa ikijihusisha na upandaji miti
ya dawa,matunda pamoja na kuhamasisha utunzaji wa vyanzo vya maji mkoani
Katavi.
Miongoni mwa makabila yanayotajwa
kuwa asilia yanayopatikana kwa wingi mkoani Katavi ni pamoja na
Wabende,wapimbwe,wakonongo,waruila na wanyakalema waliopo mwambao wa ziwa
Tanganyika.
Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa
ya Tanzania iliyokuwa na machifu na watemi katika miaka iliyopita ambapo neno
Katavi lenye maana ya MZIMU lilibadilika kutoka maneno ya awali Katabhi,Katabi
na Mpaka sasa Katavi na sababu ya kubadilika kutokana na baadhi ya watu
kushindwa kutamka maneno vizuri.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.co
Comments