MJI WA NAMANYERE NKASI KUJENGEWA LAMI KABLA YA 2020-Septemba 11,2017
SERIKALI imesema inatarajia kukamilisha ujezi wa
barabara yenye urefu wa kilomita tano kwa kiwango cha lami Mjini Namanyere
Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa kama iliyoaihidiwa na serikali wakati wa kampeni za
uchaguzi mwaka 2015.
Kauli hiyo imetolewa leo bungeni Dodoma na Naibu
waziri wa Ofisi ya Rais tawala za mikoa na Serikali za mitaa Mh.Suleiman Jafo
wakati akijibu swali la mbunge wa Nkansi Kusini Mh.Deuderit Mipata aliyetaka kujua utekelezaji wa ahadi ya rais
katika ujenzi wa miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami.
Mheshiwa Jafo amesema serikali kupitia wakala wa
barabara za mijini na vijijini Tarula anatarajiwa kutekeleza ahadi ya rais
kabla ya mwaka 2020.
Wakazi wa mji wa Namanyere ambao ni makao makuu
ya Wilaya ya Nkasi wamekuwa wakihangaika kupita katika barabara zilizopo katikati ya mji huo hasa
wakati wa masika.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments