TANROADs MKOANI KATAVI WATAJWA KUSABABISHA AJALI-Septemba 22,2017
Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
BAADHI ya wakazi wa wanispaa ya
Mpanda Mkoani Katavi wameilalamikia Wakala wa barabara TANROADs Mkoani Katavi
kwa kupuuzia uwekaji alama za usalama barabarani katika eneo la Super City mtaa
wa Majengo eneo ambalo limekuwa likisababisha ajali mara kwa mara.
Wakizungumza na Mpanda Radio katika
eneo hilo,wakazi hao wakiwemo Rajabu Ally Hussein na Ramadhan Fadhili wamesema
kila wakati ajali hutokea katika eneo hilo kutokana na kutokuwepo
matuta,mzunguko na alama nyingine zinaoonesha kuwepo kwa alama ya makutanio ya
barabara.
Taarifa kuhusu matukio ya ajali yanayoendelea
kutokea katika eneo la Super City Mtaa wa Majengo inafahamika kwa wakala wa
Barabara TANROADs kwa sababu Wiki mbili zilizopita Mhandisi wa TANROADs Mkoani
Katavi Frank Mwakisonga alidai aandikiwe barua ndipo azungumze na chombo cha
habari au vyombo vya habari ili kueleza mikakati waliyonayo kuhusu eneo hilo
hatarishi kwa wakazi Mkoani Katavi.
Eneo linalodaiwa kutokea ajali mara
kwa mara lina makutanio ya barabara tatu za Mpanda-Sumbawanga,Mpanda-Kigoma na
barabara inayoingia katikati ya mji ambapo mapaka sasa tangu barabara ikamilike
hivi karibuni,kwa mjibu wa waendesha vyombo vya moto,zaidi ya ajali tano
zimetokea katika eneo hilo na kusababisha vifo na majeruhi.
Comments